logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pasta T akiri kulala na wanawake wawili wenye virusi vya ukimwi

Kwa neema ya Mungu sikuambukizwa virusi hivyo Pasta T alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani14 November 2023 - 13:58

Muhtasari


  • •Pasta huyo alisema kuwa cha kushangaza ni kuwa wakati alipoenda kufanya vipimo vya gojwa wa ukimwi alipatikana kuwa hasi kwa neema ya Mungu
Pasta T Mwangi

Mhubiri wa kanisa la Life Church International, Mchungaji T Mwangi amesimulia jinsi Mungu alimuepesha na virusi vya ukimwi licha ya kushiriki mapenzi na wanawake wawili tofauti waliokuwa na virusi hivyo.

Mchungaji huyo alisimulia hayo huku akisema kuwa matukio hayo yalitokea kabla ya kuokoka na kuyaacha mambo ya dunia.

Anakumbuka Krismasi moja ambapo aliondoka nyumbani kuelekea klabu.

"Nilienda klabu na kitu cha kwanza kutokea ni kupigana, chupa ya pombe ikarushwa,  kwa bahati nzuri niliponea."

Kiongozi huyo wa kanisa alisimulia jinsi alivyokutana na mwanamke ambaye alifanya naye mapenzi  na baadaye akafariki kutokana na virusi vya ukimwi.

Ulikuwa ni msimu wa Krismasi, nilikuwa nimelewa na nikalala na mwanamke ambaye sikujua alikuwa na virusi vya ukimwi, baadaye tulimzika mwanamke huyo.

Mchungaji huyo alisimulia  kuingia kwenye uhusiano mwingine na mwanamke ambaye alikuwa ameambukizwa virusi na Sugar Daddy.

"Nilianza kuchumbiana na mwanamke mwingine na jambo lile lile tena likajitokeza ,Niliambiwa kuwa mwanamke alikuwa ameambukizwa virusi na "sugar daddy "na alikuwa mgonjwa,"alisema.

Pasta huyo alisema kuwa cha kushangaza ni kuwa wakati alipoenda kufanya vipimo vya ugojwa wa ukimwi alipatikana kuwa hasi kwa neema ya Mungu.

"Nilienda "VCT" kupimwa cha kushangaza  nikawa bila virusi kwa Neema ya Mungu,Jinsi Bwana alivyonihifadhi, sijui,"alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved