logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond kuandaa sherehe ya kukata na shoka yenye kauli mbiu "swahili night" kumkaribisha msanii mpya

Msanii tunayesajili ni bora zaidi ya wote Diamond asema

image
na Davis Ojiambo

Burudani15 November 2023 - 09:08

Muhtasari


  • •Diamond platnumzs ambaye ndiye mkurungezi mkuu na mwazilishi wa Lebo wasafi yumo na wasanii tajika kwenye lebo wakiwemo nyota Zuchu,Mbosso ,msanii Lava lava

Staa wa Bongo Diamond Platnumzs ametangaza Tarehe kumi na saba Novemba kuwa siku muhimu sana kwa Lebo  ya Wasafi kwani wataandaa sherehe yenye jina  Swahili night ili kukaribisha nyota mwingine kwenye lebo.

Msanii huyu kupitia kwenye mtandao wake wa instagram usiku wa kuamkia leo alichapisha taarifa hiyo akisimulia kuwa ni sherehe ambayo itakuwa na bwebwe za aina yake kumtabulisha msanii shupavu.

"Lebo wasafi litafanya sherehe ambayo hijawaikutokea popote kumtabulisha msanii mpya ndani ya kikosi chetu ni jambo la kujivunia hafla ambayo itahudhuriwa na waalikwa tu,...

Ni sherehe ya siku mbili waalikwa watakuja wakiwa wamevaa mavazi ya uswahilini zikiwemo kanga,dera,ili kuonesha dunia kuwa uswahili ndio mtindo bora wa kuigwa,"alisema.

Diamond platnumzs ambaye ndiye mkurungezi mkuu na mwazilishi wa lebo wasafi yumo na wasanii tajika kwenye lebo wakiwemo nyota Zuchu,Mbosso ,msanii Lava lava

Tangazo hili linaenda kinyume na tangazo ambalo alifanya mapema mwezi Julai alipokuwa akitoa tahadhari kwa wasanii wenzake kuhusu kuachia miziki kwa mfululizo hadi mwakani.

Akitoa tangazo hilo, Diamond alikuwa amedokeza kwamba angemtambulisha msanii mpya kwenye lebo ya Wasafi mapema Januari mwaka 2024, muda ambao angempisha msanii huyo kuchukua hatamu ya kuongoza kwenye" trend"baada ya yeye kufanya hivyo kuanzia Julai hadi sasa mfululizo bila kutikiswa.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved