Mchungaji wa kanisa la Neno Evangelical, James Ng’ang’a kwenye Video moja mitandaoni alinekana akimkashifu mshirika mmoja aliyekuwa ametoa sandaka ya mia akimtaka aombee familia yake.
Kulingana na Pasta Ng'anga' mshirika anayetoa sadaka ya shilingi mia tano inakuwa vigumu sana kumkubuka wakati wa maombi.
"Juzi kuna mama mwingine alinipea sadaka ya mia tano akaniambia niombee, watoto wake, wajukuu,na familia nzima....mia tano hata niwakumbuke namna gani sasa,hata haitoshi mafuta ya gari,"alisema.
Mchungaji huyo aliendelea kusimulia zaidi,"Hiyo mia tano pelekea wanganga ufanye maombi nao mimi siwezi kusumbua Mungu nikiombea mshirika anayetoa mia tano," alisema.
Pasta Ng'ang'a kwenye ibada na washirika wake aliagiza mmoja wa watumishi wa kanisa kuleta kikapu cha sadaka na kutenganisha thamani ya pesa kwenye kile kikapu.
"Naomba uchukue kikapu cha sadaka umwage pesa zote kwa madhabahu tenganisha elfu tu hizo zingine wacha hapo kuna watu wanamchezea Mungu wacha hata mia tano kuna wengine wametoa mia moja wanamchezo sana,'alisema.
Mchungaji huyu alisema kuwa hawezi kuendelea kufanya ibada na washirika kama hao akisema kuwa hakuna upako wa mia tano labda waende kwa wanganga.