logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond ni 'Risk taker' anawekeza kwa wasanii bila kujali -Baba levo

Diamond ni mfano wa kuigwa amejitolea sana kukuza vipawa Baba Levo asema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani17 November 2023 - 13:23

Muhtasari


  • •Msanii huyo aliwashauri wasanii wote chini ya Lebo la Wasafi na wale walijiodoa baada ya kutajirika kumpa mwazilishi wao heshima kwa kuwa alitumia hela nyingi kwa sababu ya mafanikio yao
Baba Levo na Diamond

Msanii wa Tanzania, Revokatus Kipando, almaarufu Baba Levo, amemsifia  Diamond Platnumz akimtaja kuwa 'Risk taker' mkubwa ambaye anawekeza kwa wasanii bila kujali kupoteza hela zake.

Baba levo alisema hayo wakati wa sherehe zilizoandaliwa na Lebo la Diamond Wasafi ili kumutambulisha msanii mpya kwenye Lebo.

"Diamond ni msanii wa kuigwa kwa mambo makuu anayoyafanya licha ya kuwa alipoteza hela nyingi baada ya kuwatambulisha wasanii na baada ya kung'aa wakajitoa kwa Lebo yake bado yuko na roho ya upendo kwa wasanii, ametumia hela nyingi ili kufanikisha nyota nyingi bila kujali kama hela zake zinapotea yeye anafanya hivyo kwa mapendeleo kwa sanaa",alisema.

 

Msanii huyo aliwashauri wasanii wote chini ya Lebo la Wasafi na wale wajiodoa baada ya kutajirika kumpa mwanzilishi wao heshima kwa kuwa alitumia hela nyingi kwa sababu ya mafanikio yao.

"Sidhani kuna mtu anaweza kuchukuwa hatua ya kuekeza mabilioni kwa wasanii bila kujali faida atakayopata kwake, Diamond amejaribu sana kuwa mfano bora,"alisema Baba Levo.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved