logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hatimaye Diamond amtambulisha msanii mpya kwenye Lebo lake la Wasafi

Msanii D VOICE ndiye msanii mpya  wa Lebo ya Wasafi baada ya kutambulishwa rasmi.

image
na Davis Ojiambo

Burudani17 November 2023 - 06:52

Muhtasari


  • •Diamond alisimulia kuwa nia yake kwa Kumtabulisha Msanii D VOICE ni kumlea kama mwanamziki na kuchipua nyota yake kwani ni mwanamuziki mchanga mwenye bidii na heshima
Diamond na DVoice

Mkurungezi mkuu na mwanzilishi wa Lebo ya Wasafi Diamond Platnumz alikuwa ni mwenye furaha baada ya kumtambulisha msanii mpya ili kushirikiana nao kusukuma gurudumu la muziki wa Bongo kwenye Lebo la Wasafi.

Msanii huyo 'D,Voice' alitambulishwa rasmi na Bosi wake kupitia hafla ya kufana 'Swahili Night' iliyoandaliwa ili kumkaribisha .

D VOICE  ambaye ndiye atakayekuwa  msanii mchanga sana kwenye Lebo la Wasafi atajumuika na wasanii wengine kwenye Lebo hiyo akiwemo Msanii Zuchu, Mbosso na Msanii Lavalava ambao wote wako chini ya Bosi wao Diamond.

Diamond kwenye hafla hiyo alisimulia kuwa nia yake kwa Kumtabulisha D VOICE ni kumlea kama mwanamuziki na kuchipua nyota yake kwani ni mwanamuziki mchanga mwenye bidii na heshima.

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja msanii huyo mpya wa Lebo la Wasafi alisimulia furaha yake huku  akimtaja Diamond  kuwa baba mlezi wa nyota nyingi za wanamuziki wanaochipuka.

"Nilipopata ujumbe kuwa Diamond Platinumz alikuwa na nia ya kunijumuisha kati ya wasanii wa Lebo ya Wasafi kwa kweli nilichanganyikiwa huku machozi yakinitoka kwani sikuwahi fikiria jambo kama hilo...Diamond nilikuwa namuona tu kwa Runinga ilikuwa vigumu kwangu kumfikia ila Mungu ni mwema, Hatimaye ndoto yangu ya muziki itang'aa mikononi mwake," alisema D VOICE.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved