Jamaa mmoja aliyechoka kudhalilishwa mitandaoni na marafiki zake kwa kutokuwa na ndevu amelazimika kuchukua hatua ya kukomesha kudhalilishwa kwa kufanya upasuaji wa kuwekewa ndevu.
Isipokuwa kwa masharubu madogo, mwanamume huyo hakuwa na nywele chini ya kidevu chake, jambo ambalo labda lilimfanya akose Amani ya nafsi.
Video hiyo ilichapishwa katika mtandao wa X, awali ukijulikana kama Twitter na mtumizi kwa jina, @the_Lawrenz.
Alishiriki video kwenye jukwaa iliyoonyesha wakati mwanamume huyo alifanyiwa upasuaji na sura yake mpya.
Baada ya upasuaji, ilionekana kuwa alikuwa na ndevu kamili. Mwanaume huyo alikuwa akitabasamu huku akionyesha mabadiliko yake.
Lakini je, ni utaratibu upi hufuatwa kufanikisha upasuaji wa kupandikiziwa ndevu?
Kwa mujnibu wa Healthline, Kupandikiza ndevu ni hivyo tu: Nywele huchukuliwa kutoka sehemu moja ya mwili na kupandikizwa kwenye kidevu chako na popote unapotaka ndevu zako zikue.
Daktari atahitaji kwanza kutathmini ngozi yako na nywele ili kuhakikisha kuwa wewe ni mgombea mzuri, na kisha utahitaji kuamua ikiwa ni thamani ya gharama.
Kama utaratibu wowote wa matibabu, hakuna hakikisho la asilimia 100 kwamba utafurahiya matokeo. Makovu ya kupandikiza ndevu daima ni hatari.
Lakini ikiwa unaweza kupata mtoa huduma aliyehitimu, inaweza kuwa na thamani angalau kuchunguza ikiwa saa chache katika ofisi ya daktari zinaweza kutoa ndevu za kudumu maisha yote.
Taratibu hiyo huchukua vipandikizi kati ya 2,000 hadi 5,000 vya follicle ya nywele au zaidi kutoka nyuma ya kichwa, kwa kawaida sawa na masikio yako, au chini kidogo, na kuziweka kwenye uso.
Kipandikizi ni kinyweleo ambacho hupandikizwa.