Mwanamume mwenye jinsia mbili nchini Nigeria ameripotiwa kupoteza figo zote mbili wakati wa mchakato wa kufanyiwa upasuaji wa kuongezewa makalio ili kuwa Zaidi kama mwanamke – mchakato ambao ulienda fyongo.
Jamaa huyo ambaye ni maarufu kwa masuala ya fasheni alifahamika kwa jina la Daniel Anthony Nsikan, maarufu kama Jay Boogie ambaye wengi wanamfahamu kupitia usosholaiti wake mitandaoni.
Kwa mujibu wa toleo la Daily Post la nchini humo, Loveth Jennifer, daktari na rafiki wa karibu wa Jay Boogie, alifahamisha haya katika chapisho la mtandao wa kijamii siku ya Ijumaa.
Akitangaza kupitia Instagram story, aliandika: "Katika hatua hii, Jayboogie anahitaji kupandikizwa figo. Figo zote mbili zimefeli. Tuliomba na kutamani isifike katika hatua hii lakini ndiyo hii. Nitatoa sasisho zingine hivi karibuni."
Jay Boogie, wiki mbili zilizopita, katika video iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii, alimkosoa daktari wake kwa kumfanyia upasuaji ambao haukutekelezwa vizuri ambao ulitishia maisha yake.
Upasuaji huo ulioshindikana ulisababisha kushindwa kukojoa kwa takriban wiki tatu sasa.
“Maisha yangu yalibadilika, hata sinifahamu tena na nimekuwa nikikabiliwa na matatizo ya kuumia figo na mengine mengi. Nimekuwa na plasmapheresis bado sijaimarika 😢 matokeo ya vipimo yanaonyesha afya yangu inadhoofika 😢 nahitaji msaada wa dhati na wa haraka,” Jay Boogie alichapisha kwenye Instagram yake siku tatu zilizopita.