Siku moja baada ya matokeo ya mtihani wa darasa la nane KCPE kutangazwa mwanablogu wa mitandao almaarufu Thee Pluto amejitokeza huku akisema kuwa yuko na nia ya kusaidia mmoja kati ya wanafunzi waliofanya mtihani huo.
Muunda maudhui huyo alisema hayo baada ya kushapisha ujumbe kupitia mtandao wake wa Instagram.
"Natafuta mmoja wa wanafunzi ambao wamefanya vyema kwenye mtihani wa mwaka huu ili kuweza kutimiza ndoto zake ya kujiunga na shule ya upili, lazima awe kati ya wanafunzi ambao wanatoka kwa familia ambaz haziwezi kujikimu kimaisha ,familia ambayo hiwezi kuwa na uwezo wa kusomesha,"alisema Thee Pluto kupitia ujumbe wake kwenye mtandao.
Mwanablogu huyo aliwaomba Wakenya kumsaidia kutafuta mmoja wa wanafunzi hao na kuwasilisha ujumbe kwenye mtandao wake.
"Ikiwa unamfahamu mmoja kati ya wanafunzi ambaye alifanya vyema kwenye mtihani wake naomba muweze kuwasilisha majina yake na matokeo kwenye "DM" yangu alisema.
Mwanablogu huyo amekuwa wa kwanza kujitokeza mitandaoni akiwa na nia ya kumfadhili mwanafunzi yeyote ili kumuwezesha kujiunga na shule ya upili.
Matokeo ya KCPE mwaka huu yamekuwa ya mwisho baada ya kukamilika kwa mtaala wa 8-4-4