Siku chache baada ya wapenzi wawili mwanamuziki Akothee na mpenziwe Omosh kutengana baada ya kuandaa harusi ya kifahari, mhubiri aliyefugisha ndoa hii amefunguka na kusimulia jinsi alizipokea habari hizo.
Mchugaji Welly Odendo kama alivyojitabulisha kwenye mohojiano ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao alisimuli kuwa Kuachana kwa wawili hao kulikuwa kwa hiari yao kwani wao wenyewe ndio walijua masaibu yaliyochangia kuachana kwao.
Hata hivyo mchugaji huyo alisema kuwa kuna haki ya kila mwanandoa kufanya jambo ambalo litaridhisha maisha yake huku akisema kuwa ikiwa ndoa imeshidikana uamuzi wa talaka hutoka kwa wenye ndoa.
"Akothe na Omosh ikiwa walikaa chini wakaona ndoa yao haitafanya kazi hayo ni kulingana na wao wenyewe kwani ndoa ilikuwa juu yao tu hawakufanya kwa ajili ya mtu mwingine," alisema.
Kulingana na mchungaji huyu vyombo vya habari ndivyo vinachukulia jambo hilo kama jambo la kwao ila haliwahusu kwa vyovyote vile kwani ikiwa wawili wameshidwa na ndoa talaka ni kwa manufaa yao.
"Wanahabari wanachukulia ndoa ya Akothee kama yao wanachochea mpaka ikakuwa taarifa kubwa ambayo imekuwa kauli ya kila siku,"alisema mchugaji huyo.
Kwenye mahojiano hayo na wanablogu mhubiri huyo aliwashauri wambea kuwachana na ndoa ya Akothee na aliyekuwa Mpenziwe Omosh na kuwatakia mema kwa kuna sababu ambayo ilichangia kusabaratika kwa ndoa yao.