Mcheza santuri Pierra Makena ni mama mwenye furaha baada ya bintiye wa miaka 7 kupata kazi yake ya kwanza kama muigizaji wa filamu.
Pierra alitumia Instagram kushiriki habari hizo na mashabiki wake, akisema kwamba anashukuru kwa timu ambayo iliweza kutambua talanta ya Ricca.
Ricca atashirikishwa pamoja na mwigizaji na mchekeshaji Jackie Vike, ambaye ni maarufu kwa jina la Awinja Nyamwalo. Maelezo kuhusu filamu bado ni machache.
"Wakati wangu wa machozi ya furaha. Ricca amewahi dili lake la kwanza kuigiza filamu na ninajivunia yeye. …. Siwezi kueleza jinsi ninavyoshukuru kwa timu ya waigizaji na wakurugenzi/watayarishaji kwa kuona talanta katika msichana wangu mdogo… yuko mbali nami kwa siku 4 na hata sijui jinsi ninavyohisi…. Pia ninajua atakuwa anaigiza pamoja na Jackie Vike kwa hiyo nimetulia kidogo☺️ #hongera mtoto wangu @riccapokotofficial,” mama mwenye furaha alinukuu video akiwa na bintiye.
Katika video hiyo, alipa kwaheri Ricca akiondoka alipokuwa akichukuliwa na basi kuelekea kwenye shughuli ya kuigiza kwa siku 4.
Itakumbukwa hivi majuzi Makena alisema kwamba hayuko tayari kuweka wazi jina la baba bintiye lakini akasema kwamba wamewahi kutana mara moja moja.
Makena alifichua kwamba bintiye ni msumbufu kwa maswali ya mara kwa mara kuhusu uwepo wa babake lakini naye akasema ana uwezo wa kuyamudu maswali hayo kwa kumdanganya kuwa amesafiri – uongo ambao hata hivyo alikiri kwamba hatokuja kuendelea kumdanganya bintiye kwa maisha yake yote.
“Wakati anauliza maswali kama hayo kuhusu babake, ana wazo kwa mbali kuhusu babake lakini maswali ambayo anauliza ni ‘lakini niliwahi kumuona, wa hiyo ako wapi?’ lakini wakati anauliza huwa namjibu unajua ‘babako alisafiri’ au ‘ako tu bize atakuja mkutane ako mbali kikazi’… huwa najaribu kukwepa masuala kama hayo lakini pia huwa najaribu kumhakikishia kwamba ‘unajua babako anakupenda’ ili tu kuhakikisha kwamba haimuathiri kwa njia hasi,” alisema katika mahojiano na Mungai Eve.
“Naamini wakati atakuwa mtu mzima, atajua dunia ikoje, na natumai hatokuja kulifikiria kwa njia hasi.” Aliongeza.