Mwimbaji mzaliwa wa Pwani Fredrick Mutinda almaarufu Brown Mauzo amefichua kuwa aliyekuwa mke wake, Vera Sidika alibadili dini na kuwa Muislamu ili kuuvutia moyo wake.
Katika mahojiano na Nairobi News, Mauzo alitambua uamuzi wa mama huyo wa watoto wake wawili wa kubadili dini kama kitendo maalum na ishara ya upendo.
Kulingana na mwimbaji huyo, Vera Sidika alichukua uamuzi wa kubadilisha dini yake kwa ajili ya ndoa yao ili wawe wanandoa Waislamu.
"Siku moja, alinipigia simu akielezea nia yake ya kubadili dini na kuwa Muislamu akisema anataka tuwe wanandoa Waislamu. Hii ilikuwa ni dhabihu muhimu aliyoitoa kwa ajili ya uhusiano wetu na nikakubali,” Brown Mauzo alisema.
Mwanamuziki huyo alifichua kwamba baada ya mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 34 kusilimu, alichukua jina la ‘Zara.
"Kitendo hiki kiligusa sana moyo wangu, na nikagundua ukweli nyuma ya nia yake katika uhusiano wetu, ingawa mwanzoni, nilikuwa na mashaka, nikishuku kuwa inaweza kuwa ya kiki ... Ujio wa kipengele cha kidini ulinifanya nichukue uhusiano wetu kwa uzito," alisema. .
Mwanamuziki huyo mzaliwa wa pwani ambaye kwa sasa ametengana na mama huyo wa watoto wake wawili alifichua kuwa ndoa yao iliisha Juni mwaka huu lakini alisubiri hadi mwezi Agosti ili kutangaza. Wawili hao walikuwa pamoja kwa zaidi ya miaka miwili na hata walikuwa wamejaliwa watoto wawili pamoja, msichana na mvulana.
Mwishoni mwa mwezi Agosti, Brown Mauzo alitangaza kuwa yeye na Vera wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.
"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.
"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.
Alishukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.
“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"