Khaligraph awasihi Wakenya wamuombee Munga huku akimtakia afueni ya haraka “Ombeeni kijana!”

Khaligraph alimtakia rapa huyo mwenzake nafuu ya haraka na kuwaomba mashabiki wamuombee.

Muhtasari

•Mwanamuziki Khaligraph Jones ameandika ujumbe wa kumliwaza rapa mwenzake Domani Munga wa Kundi la Wakadinali.

•Katika ujumbe wake mapema wiki hii, Munga alisema kwamba angepumzika ili kuzingatia afya yake.

Khaligraph na Munga
Image: INSTAGRAM// KHALIGRAPH JONES

Mwanamuziki maarufu wa Kenya Khaligraph Jones ameandika ujumbe wa kumliwaza rapa mwenzake Domani Munga wa Kundi la Wakadinali.

Siku ya Jumatano asubuhi, rapa huyo ambaye ni maarufu kwa jina la OG alichapisha picha zake kadhaa akiwa na Munga kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Katika maelezo ya picha hiyo, Khaligraph alimtakia mwanamuziki huyo mwenzake nafuu ya haraka na kuwaomba mashabiki wamuombee.

“Pona haraka, ombeeni kijana!” Khaligraph aliandika.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mwanabendi huyo muhimu wa kundi la Wakadinali kutangaza kuwa atapumzika mwezi mzima wa Disemba.

Katika ujumbe wake mapema wiki hii, Munga alisema kwamba angepumzika ili kuzingatia afya yake.

"Kutokana na suala langu la afya, sitakuwa karibu, hadi January. Poleni sana mashabiki wangu. Napata mapumziko," Munga alisema kwenye Twitter.

Wiki chache zilizopita, Wakadinali walitangaza watakuwa na shoo yao iitwayo 'Rong Experience' mnamo Desemba 15.

Munga tayari ametangaza ni lazima shoo iendelee.

"Rong Experience itakua moto na au bila mimi."

Munga ni mwanachama muhimu wa kundi la rap la Wakadinali ambalo linajumuisha yeye, Scar na Sewersydaa. Watatu hao ni miongoni mwa rapa tajika zaidi nchini Kenya pamoja na Khaligraph, Octopizzo, Burukylyn miongoni mwa wengine.