YouTuber Diana Marua ni mama mwenye furaha baada ya kubaini kwamba mwanawe wa kufikia, Morgan Bahati hivi karibuni atafikisha umri wa miaka 14.
Marua kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii alionesha jinsi anavyompenda na kumuenzi kijana huyo licha ya kuwa si mtoto wake wa kumzaa.
Alimsifia akisema kwamba haamini jinsi ambavyo muda umesonga kwani ni miaka michache tu iliyopita alipata kujuana naye baada ya kuingia katika maisha ya msanii Bahati na kumpata akiwa na mtoto huyo baada ya kumuasili kutoka kwa boma la kulea watoto wasio na wazazi.
Marua alifichua kwamba Morgan hivi karibuni atafikisha miaka 14 na kumpa maua yake kwamba ndiye pixha halisi ya kile wanawake wengi wanataka kwa mwanamume – urefu, weusi na utanashati.
“Mama wa tineja 😍Siamini mwanangu @morgan_bahati atafikisha miaka 14 ndani ya siku chache! Asante Mungu 🙏🏼 Ufafanuzi wa Kweli wa Mrefu, Mweusi na Mtanashati😍 Muda unakwenda wapi? Nakupenda Mtoto Wangu ❤️” Diana Marua aliandika kwenye picha hizo ambazo walikuwa wamevalia mavazi rangi nyeusi za kupendeza.
Hii si mara ya kwanza Diana Marua kuonesha mapenzi kwa kijana huyo.
Itakumbukwa siku chache nyuma alipakia picha za pamoja na Morgan, picha ambazo zilimburuza vikali mitandaoni kwa kumhusisha mtoto huyo na mwanasoka aliyekuwa mpenzi wa Marua, Victor Wanyama huku pia wengine wakimtupia povu zito kwa vazi lisilo la kiheshima alilokuwa amelivalia wakati wa kupigwa picha na Morgan.