logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jackie Matubia atambulisha mpenzi mpya miezi baada ya kuachana na Blessing Lung'aho (+picha)

Matubia na mpenziwe walionekana kwenye bwawa la kuogelea huku mwanaume huyo ambaye hajafahamika akimbusu mashavuni.

image
na Samuel Maina

Burudani09 December 2023 - 05:46

Muhtasari


  • •Matubia na mpenziwe walionekana kwenye bwawa la kuogelea huku mwanaume huyo ambaye hajafahamika akimbusu mashavuni.
  • •Julai, Bi Matubia alishangaza taifa baada ya kutangaza kuwa yeye ni "single mother mwenye fahari wa watoto wawili."

Muigizaji maarufu wa Kenya Jackie Matubia ameonekana kumtambulisha mpenzi wake mpya, siku chache tu baada ya kudokeza kuhusu kutaka kuolewa.

Siku ya Ijumaa, mama huyo wa watoto wawili ambaye alitengana na muigizaji mwenzake Blessing Lung’aho miezi kadhaa iliyopita alishiriki video zake akiwa likizoni Pwani na mwanamume asiyejulikana. Hata hivyo hakufichua sura nzima ya mpenziwe mpya lakini alionyesha sehemu ya mwili wake.

Katika video hizo, wapenzi hao wawili walionekana kuwa na furaha pamoja na walionekana wakifurahia nyakati za kimapenzi.

"Jinsi tunavyotulia tunaposubiri tukio letu lijalo," Bi Matubia aliandika chini ya video moja iliyomwonyesha yeye na mwanamume huyo wakiwa wamelala kitandani.

Katika video nyingine iliyoshirikishwa na mwigizaji huyo wa zamani wa Tahidi High, walionekana kwenye bwawa la kuogelea huku mwanaume huyo ambaye hajafahamika akimbusu mashavuni.

Bi Matubia alificha sehemu ya uso wa mwanamume wake mpya kwa emoji za mapenzi na kuambatanisha video hiyo na wimbo wa mapenzi wa Nyashinski ‘Perfect Design.’

Haya yanajiri takriban miezi mitano tu baada ya mama huyo wa watoto wawili kutengana na mzazi mwenzake, Blessing Lungaho ambaye ana mtoto mmoja naye.

Mnamo mwezi Julai, Bi Matubia alishangaza taifa baada ya kutangaza kuwa yeye ni "single mother mwenye fahari wa watoto wawili."

Mwezi uliopita, muigizaji huyo alizidiwa na hisia za uchungu wakati akisimulia kuwa amekuwa akiwalea mabinti zake peke yake pasi na kusaidiwa na baba zao.

Matubia alisema haya kwenye YouTube Channel yake ambapo alizungumzia kwa undani kilichomfanya kuondoka katika uhusiano wake na muigizaji huyo mwenzake waliyekutana kwenye kipindi cha Televisheni kilichokamilika mapema mwaka jana.

Mama huyo wa mabinti wawili kutoka kwa baba tofauti alizua dhana kwamba Blessing Lung’aho hawajibiki katika kumsaidia kulea binti yao baada ya kuachana miezi michache iliyopita.

Matubia alisisitiza kwamba maisha yake tangu kuachana na Lung’aho hayajakuwa rahisi na kwamba ni Mungu tu amekuwa akimshikilia muda wote.

“Mungu kwa kweli amekuwa katika kitovu cha maisha yetu, mimi na mabinti zangu, amenishikilia sana wakati kila kitu katika maisha yangu kilikuwa kinasambaratika. Mungu alinishika mkono na kunipa hakikisho kwamba yeye ni Alfa na Omega. Amekuwa baba kwa wanangu na amekuwa nguzo ya kuegemea,” Matubia alisema.

“Umekuwa ni wakati mgumu sana, miezi kadhaa iliyopita nimepitia moto na kusema ukweli nimeona mkono wa Mungu,” aliongeza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved