logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Kule kwingine kuna kunguni!" Akothee adokeza kuolewa na Nelly Oaks, kumzalia huku akimtupia vijembe Omosh

"Hapa niacheni nikae hapa kule kwingine kunguni wengi πŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ€£πŸ€£," alisema.

image
na Samuel Maina

Burudani14 December 2023 - 11:25

Muhtasari


  • β€’Akothee alidokeza kuwa sasa yuko tayari kuolewa rasmi na meneja huyo wake ambaye pia anaaminikaa kuwa mpenzi wake.

Mwimbaji na mfanyibiashara maarufu wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee amedokeza kuhusu mipango yake mikubwa na meneja wake Nelly Oaks.

Wakati alipokuwa akimsherehekea kutokana na jukumu alilocheza kwenye sherehe ya kufuzu kwake iliyofanyika Migori mnamo Desemba 10, mama huyo wa watoto watano alidokeza kuwa sasa yuko tayari kuolewa rasmi na mwanamume huyo anayeaminika kuwa mpenzi wake.

Isitoshe, pia alidokeza kuhusu kupata mtoto naye.

"Hutamuona kwenye picha nyingi kwa sababu alikuwa na shughuli nyingi za kuzunguka ili kuhakikisha kuwa malkia yuko sawa.

Pili, hakuwa akijisikia vizuri, Mpermanent wangu aliugua mafua siku ya kuhitimu kwangu lakini alifanikiwa,” Akothee alisema kwenye Facebook.

Aliambatanisha taarifa hiyo na picha zake na Nelly oaks ambaye alivalia nguo zinazofanana na gauni lake la kuhitimu.

“Nakupenda HNO. Sasa Nimesoma graduation ndio hiyo ,bado harusi na mtoto tu sweetie 🀣🀣.. Mpigieni makofi Bwana Meneja Nellyoaks,” alisema.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 aliendelea kuzungumzia kwa ufupi jinsi mwaka wa 2023 ambao unakaribia kuisha umekuwa na alijivunia kuwa yuko karibu kuukubali.

Wakati huohuo, alionekana kuitupia vijembe ndoa yake iliyovunjika na Denis Schweizer ‘Omosh’ huku akibainisha kuwa yuko sawa na Nelly Oaks.

"2023 umekuwa MWAKA wa kutatanisha ajabu lakini tuliokoka mpenziπŸ’ͺ. Hapa niacheni nikae hapa kule kwingine kunguni wengi πŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ’ƒπŸ€£πŸ€£," alisema.

Mwezi uliopita, mwanamuziki huyo alionekana kuthibitisha kufufuka kwa mahusiano yake na meneja wake wa muda mrefu Nelly Oaks katika kipindi cha moja kwa moja cha hivi majuzi kwenye mtandao wa TikTok.

Katika kipindi hicho ambacho alikuwa akiwahutubia mashabiki wake Nelly Oaks akimwandalia chakula maalum jikoni, Akothee alisikika akimwita meneja huyo wake ‘babe’ mara kadhaa, jina ambalo hutumika sana sana  wapenzi.

Nelly Oaks pia alisikika akimtaja Akothee kama mtu maalum kwake huku wawili hao wakishiriki matukio ya kimapenzi kwenye kamera.

“Hiki ni chakula cha jioni maalum kwa mtu maalum kama wewe. Ni surprise,” Nelly Oaks alisikika akimwambia mwanamuziki huyo.

Wakati wa kipindi hicho, Akothee kwa hasira aliwasuta wanawake wote waliokiri mapenzi yao kwa meneja huyo wake akidokeza kuwa hapatikani kwao.

Wakati baadhi ya mashabiki walipotaka kujua iwapo Nelly Oaks ana mchumba, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alionekana kuthibitisha kuwa yeye ndiye anashikilia nafasi hiyo.

“Ati kama Nelly ako na mtu?! Kwani mimi mawe? Mimi mawe? Ama mimi ni mti? Unauliza kama Nelly ako na mtu, kwani mimi ni mawe? Ama kijiti? Usinipimie pumzi. Maisha ni ya kwangu nayaendesha vile nataka,” alisema.

Mama huyo wa watoto watano pia alikataa ombi la nambari ya simu ya Nelly Oaks huku akifichua kwamba hata ana uwezo wa kufungua na kutumia simu yake.

“Kweli nikupatie namba ya Nelly? unadhani mimi nimetosheka? Mimi sijarudi soko, mimi ndiye soko, sigawani na mtu,” Akothee alisema.

Nelly Oaks pia aliweka wazi kuwa hapatikani kwa mwanamke mwingine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved