Sajili mpya wa lebo ya muziki ya WCB Wasafi, Dvoice Ginni amesaini mkataba wa dili nono la balozi wa mauzo ya biashara mwezi mmoja tu baada ya kusainiwa na kutambulishwa kwenye lebo.
Msanii huyo alipata ubalozi wa kuitangaza mchezo wa Kamari wa Kibubu cha Sikukuu, ikiwa ni mwezi tu baada ya kutambulishwa na alikuwa an furaha ghaya.
Dvoice alifichua ukweli wake kwamba ni kiasi kikubwa sana cha hela alichopokezwa kama balozi, akikitajak uwa kiasi ambacho hajawahi kukishika mikononi mwake tangu alipozaliwa.
“Ningependa kuwashukuru watu wote pia na uongozi wangu wa WCB Wasafi ni nguvu kubwa sana, support yao kubwa sana imefanikisha. Wamenifurahisha sana na ndio mimi pia ninafurahia nao. Niseme ni bahati tu kwa Mung, riziki zinakuja kwa bahati, ukiangalia ni dili ambalo nimesaini hela nyingi ambazo toka nianze maisha yangu ya muziki, na sio muziki tu, toka nimezaliwa sikuwahi kuzishika,” Dvoice alisema.
Pia aliutambua mchango mkubwa wa wasanii wenzake kwenye lebo – Zuchu, Mbosso na Lavalava akisema kwamba wamempa shavu kwa njia ya kipekee kuhakikisha kwamba anapata kutulia na kumakinika katika kazi za kutunga mashairi.
“Ukiangalia, tunaona kabisa mashabiki wanaona ni mwezi mmoja tu nafanya vizuri, ukiangalia wakubwa wangu ambao wako kwenye lebo nimewakuta, wamepambania mdogo wao niendelee kufanya vizuri Zaidi, kwa hiyo ina maana hakuna sababu yao kuchukia kwa nini nikapata mimi,” alisema.