Kwa mara ya kwanza tangu waoane miaka miwili iliyopita, YouTuber Thee Pluto na mpenzi wake Felicity Shiru hawatasherehekea shamrashamra za sikukuu ya Krismas pamoja.
Hii ni baada ya Pluto kufichua kwamba amejiandaa kuondoka kwenda safarini, ambapo atakuwa anazuru mataifa 5 ya Afrika Mashariki kwa ziara ya siku 15.
Thee Pluto aliweka wazi hilo katika podikast ya Felicty Shiru siku moja iliyopita akisema kwamba hatosafiri kwa ndege bali alikuwa amejiandaa kutumia barabara kuzunguka mataifa ya Uganda, DRC, Rwanda, Burundi, Tanzania na kurudi nchini Kenya katika siku hizo 15.
“Jamani mnajua kwamba katika biashara ni lazima kujinyima, na hii ni moja ya dhabihu kubwa nitakayolazimika kufanya mwaka huu,” aliwaambia mashabiki wake.
Anasema kwamba kujua kwamba hataweza kusherehekea Krismasi pamoja na familia yake mwaka huu ni kidonge kigumu kumeza lakini akasisitiza kuwa itakuwa ni kujidhabihu.
Felicity pia alichukua YouTube yake na kuunda video akielezea kuwa tayari alikuwa amemkosa mume wake saa chache baada ya kuondoka.
Mama huyo wa mtoto mmoja alieleza kuwa alikuwa akitafakari jinsi atakavyotumia msimu wa Sikukuu bila yeye kwani walikuwa wameshapanga mipango.
“15 days is gonna be long time, 15 days na venye kuna njeve,” alitania.
MwanaYouTube huyo maarufu alijizolea umaarufu alipoanzisha Kipindi chake cha Mtihani wa Uaminifu kwenye Youtube ambapo aliwashirikisha wanandoa, akiwafichua wadanganyifu kipindi ambacho kilivutia watazamaji zaidi, ambao walikaririshwa na video zake kwa furaha na drama.