Katika miaka ya hivi karibuni, ulaghai wa mapenzi haswa katika ndoa pamoja na usaliti limekuwa jambo la kawaida sana ambalo linatekelezwa na wanaume na wanawake.
Wakati huo huo pia kumekuwa na fumanizi nyingi ambazo hupelekea matokeo ambayo si ya kufurahisha, ikiwemo mauaji kutokana na hasira lakini pia mtu kujiua baada ya kuhisi moyo wake kuchezewa shere.
Lakini janaa mmoja ameibuka na mbinu mpya kabisa ya kulipa kisasi baada ya kumfumani mke wake akichepuka na mwanamume mwingine.
Katika picha za mwanamume huyo ambazo zilishirikiwa kwenye mtandao wa X na mtumizi mmoja kwa jina @PeopleWithIQ, mwanamume huyo baada ya kuwafumani, hakuwadhuru kwa njia yoyote kimwili, bali aliamua kuwadhuru kisaikolojia Zaidi, kivipi?
Mwanamume huyo alipomfumania mkewe akishiriki mapenzi na mwanamume mwingine, alichukua picha zao na kuondoka nazo kisha akazichapisha kwenye upande wa mbele wa Tsheti yake.
Mwanamume huyo wala hakuishia hapo, baada ya kuchapisha picha hizo kwenye Tsheti, aliamua kufanya ziara ya kumtembelea mkewe katika ofisi ambako alikuwa anafanya kazi, akiwa ameivaa Tsheti hiyo.
Picha za T-shirt zimeenea kwenye mitandao ya kijamii, na kusababisha mijadala kuhusu mahusiano, ukafiri, na jinsi watu wanavyokabiliana na maumivu ya kihisia kwa njia tofauti.
Chapisho hilo linasema, “Mwanaume huyu alimshika mkewe akichepuka. Akawapiga picha, akaiweka kwenye fulana na kwenda kumuona kazini akiwa amevaa shati hilo”.
Chapisho hilo limevutia hisia mseto, baadhi wakimkosoa kwa kuamua kumdhalilisha mkewe hadharani hadi maeneo yake ya kazini.
Lakini wengine pia walimsifia kwa kutochukua maamuzi magumu ya kumuumiza au kuwajeruhi alipowafumani, na badala yake kuchukua msimamo tofauti kabisa wa kuwafanya wahisi uchungu pasi na kuwadhuru kimwili.