Aliyekuwa mpenzi wa mchekeshaji Mulamwah, muigizaji Carrol Sonie ametangaza kuwa harusi yake itafanyika Jumamosi hii ya Januari 6.
Sonie ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akionekana kuzua ushindani na babydaddy wake tangu asikie anatarajia mtoto pamoja na mpenzi wake mpyac Ruth K, alifichua haya kupitia Instastory yake.
Akitangaza tareeh hiyo ya harusi yake, Sonie alimshukuru Mungu kwa kumuongoza katika penzi lake na mwanamume ambaye hajawahi kumfichua kwa umma tangu mwaka jana alipodokeza kuwa ameshapata wa kuziba pengo lililoachwa na Mulamwah katika mtima wake.
“Ni tarehe 6 Janauri,” Sonie aliandika na kuambatanisha na emoji ya mapenzi, pete na bibi harusi. “Mungu amekuwa mwema kwangu, je umealikwa?” aliuliza.
Tangazo hili linakuja wiki chache tu baada ya Mulamwah na mpenzi mpya Ruth K kufanya kile kilichotajwa kuwa ni harusi ya kitamaduni nyumbani kwao.
Mulamwah na Ruth K walionekana wenye furaha wakichezesha mabega kwa mbwembwe katika hafla hiyo ambayo walikuwa wamevalia vitenge sawia.
Baadaecwalikuja kutangazia umma kwamba wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja na hivi majuzi walishiriki video ya kufichua jinsia ya kijacho.
Kwa upande wake, Sonie amekuwa akisisitiza kwamba Mulamwah hajawahi kumsaidia katika malezi ya mwanao, akisema kwamba amekuwa akipitia kipindi kigumu sana kumlea mtoto ambaye anamfanana baba ambaye alimkataa.
“Sijui kama inauma ama nini, lakini mashabiki wangu, haswa kina mama, hebu tafakari kulea mtoto wako ambaye amekataliwa halafu sura yake ni ya babake? Unafanya nini katika hali kama hiyo? Unajipa moyo na kusonga mbele haijalishi,” Sonie alisema katika video aliyoichapisha kwenye YouTube yake mwezi mmoja uliopita.