Muigizaji mkongwe wa Bongo, Jacqueline Wolper amesema kwamba anatamani kumaliza kuzaa akiwa na miaka 40 ili kuanza kujishughulisha na mambo menine kimisha.
Wolper ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 35 na mama wa watoto wawili kupitia mitandao ya kijamii alisema kwamba ndoto yake ni kuanza safari ya kuwalea wanawe tu pindi atakapovuka umri wa miaka 40.
Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond na Harmonize alifunga harusi ya kufana mwaka jana na tajiri Rich Mitindo na mpaka sasa wanawatoto wawili.
Kwa ndoto zake, Wolper anataka kuanza kujituliza akijivinjari na maisha mbali na uzazi wa kubeba ujauzito akiwa na umri huo.
"Natamani Mungu anijaalie nikifikisha miaka 40 niwe nimemaliza kuzaa, niwe nimemaliza majukumu yote ya mihangaiko nibaki na kazi ya kulea, kula bata la uhakika. Mungu nipe uhai na Afya njema," Wolper alisema.
Wolper ni mmoja wa warembo waliofanikiwa pakubwa kwa kuiweka tasnia ya uigizai Tanzania kwenye ulingo tangu mwaka wa 2007.
Waigizaji wenzake ambao walianza nao ni pamoja na Wema Sepetu, Irene Uwoya, Aunty Ezekiel miongoni mwa wengine ambao ujio wa Instagram pia uliwapa msukumo mkubwa kwa kujiendeleza kama wanasosholaiti lakini pia wajasiriamali katika fani mbalimbali.
Kati ya rafiki zake hao, Wolper ndiye pekee ambaye amebahatika kuipata ndoa takatifu kwa maana ya kufunga harusi rasmi.