Msanii Stevo Simple Boy amezua utani mitandaoni baada ya kuomba kupewa mafunzo jinsi ya kukuna.
Katika Instagram yake, alipakia video akiomba jamaa anayejiita ‘Bwana Mkunaji’ kumfuata ili kumpa mafunzo ya kukuna kwa sababu lengo lake kuu katika mwaka wa 2024 ni kujua jinsi ya kukuna.
“Kuna mtu anajiita bwana mkunaji, mimi kama Stevo Simple Boy naomba aje anifunze jinsi ya kukuna kuna. Huu mwaka wa 2024 nataka kukuna kuna kunakuna. Tafadhali, njoo bwana mkunaji unifunze jinsi ya kukuna kuna, au sio, ndio maanake,” Stevo Simple Boy alisema.
Hata hiovyo, kwenye upande wa kutoa maoni, baadhi ya watu walihisi alikuwa anamchokoza msanii Willy Paul ambaye katika siku za nyuma alikuwa anajitambulisha kwa msimbo ‘Bwana Mkunaji’.
Hata hivyo, Pozee baadae mwaka jana alidondosha msimbo huo akisema kwamba asingependa tena kuendelea kutambuliwa na mashabiki hivyo kutokana na dhana mbaya ambayo ilikuwa imeanza kuhusishwa na msimbo huo.
“Utagongwa na pozee ww” Salma Abdallah.
“willy Paul onyesha uyu kukuna” Pracydea.
“@willy.paul.msafi Habari do hiyo” Ricks Musyio.
Hii inakuja siku chache baada ya msanii huyo kudai kwamba angependa kurejelea katika miziki ya injili baada ya kupungwa na wimbo wa Bunny Asila na Christina Shusho.
Hata hivyo, hajaonekana kutii neno lake kwani hivi majuzi tena alionekana kujiingiza katika uanaharakati baada ya kudokeza kionjo cha wimbo wake wa kiharakati kuhusu baa la njaa na jinsi serikali imekuwa ikiwakandamiza walala hoi.
“Wakenya kweli twateseka watoto wanalala bila chakula, bei kweli imepanda hata za vyakula, sasa imekuwa tabu kula, serikali imekwepa kutupa mahindi, watu wachomeka kwa duka la wahindi, Wakenya mbona tusiwe washindi…” sehemu ya mistari ya wimbo huo wa kiharakati iliimba.