Mchekeshaji ambaye pia ni YouTuber, 2Mbili amejitokeza na kunyoosha maelezo baada ya baadhi ya watu mitandaoni kumhusisha na mtu ambaye msanii Willy Paul alikuwa anazungumzia hivi majuzi kuwa amekuwa akiwaambukiza wasichana virusi vya UKIMWI.
Akizungumza na waandishi wa habari za mitandaoni, 2Mbili alisema kuwa japo wengi walikuwa wanahisi ni yeye Willy Paul alikuwa anatumbua, madai hayo ni ya uongo na hayana msingi kwani Pozee hakutaja jina la mtu katika ufichuzi wake.
Willy Paul aliandika kwenye Instastory yake kuwa kuna celeb ambaye ni mchekeshaji anayetumia fursa yake kuwaambukiza wasichana wenye kati ya umri wa miaka 18-25 UKIMWI pasi na wao kujua.
“Sijui ni nani, pengine ni mimi kwa sababu natumia muda mwingi na Willy Paul, kwa hiyo sidhani hata kama ni mimi ndio napeana hivyo virusi. Willy Paul sijui anaezakuwa ananijua aje ama ameambiwa na watu wenye pengine tushawapea. Wacha watu wajieleze, ni vizuri, kama ni 2Mbili wacha wanitag,” Mchekeshaji huyo alisema.
Alikwenda mbele na kuongeza kuwa hata kama angekuwa ni yeye mwenye virusi, asingependa kuwaambukiza watu wasiojua kwani ana ufahamu fika kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
“Najua ni haramu kulala na mtu kama unajua hali yako ni chanya, bila kinga. Ni uhalifu unaeza hata kufungwa maisha yote. “Wale wasee wanadhania ni 2mbili its good for them, I know myself mimi siwezifanya hivyo ati kuinfect ugonjwa huu and me mwenyewe najua its illegal. Simaanishi ati niko nayo hata kama niko nayo ni yangu, inakuathiri hata kidogo,” 2Mbili alisema kwenye mahojiano.
2Mbili pia alimtetea Willy Paul akisema kuwa alifanya vizuri kuanika celeb huyo kama njia moja ya kuwaokoa wasichana lakini pia akampa changamoto ya kwenda Zaidi kumfuata celeb mwenyewe na kumwambia kuwa hapendi matendo yake.
“Ilikuwa vizuri pia kwa umma kujua sasa ni kwa ajili yake kwenda kwa mtu kama 2mbili aje aambie 2mbili ‘sipendi wewe unaambukiza mwili wetu magonjwa hayo. Ni vyema aende moja kwa moja kwa mtu huyo coz jinsi anavyoipunguza, alianza ni celeb, akakuja msanii, mcheshi sasa hata wale wanamuziki waliridhika, kidogo atasema ni wacheshi wa TikTok,” baba wa watoto watatu alisema.