Msanii Harmonize kutoka lebo ya Konde Music Worldwide amemshangaza mpishi wake wa nyumbani, Zuwena baada ya kumuandalia bonge la tafrija ya kusherehekea mimba yake maarufu kama babyshower kwa lugha ya kukaza meno na kulegeza ulimi.
Kupitia Instagram stories zake, Harmonize aliandaa tafrija hilo nyumbani kwake wakiwa pamoja na mpenzi wake mpya, Poshy Queen.
Alifichua kwamba mpishi wake wamejuana kwa takribani miaka 8 na ilikuwa vizuri kumuandalia tukio la kumfanya ajihisi kufarijika.
Harmonize ambaye kwa muda amekuwa akimtaja Zuwena kwenye video zake na hata kufanya video naye wakiwa nyumbani alimpa umaarufu kwa kiasi Fulani mrembo huyo ambaye kundi zima la Konde Gang linamchukulia kama familia.
Alimtania kwamba nyumbani amekuwa akiweka ulinzi kumbe alikuwa anaishi na wahuni, akiashiria kwamba huenda ujauzito huo ni wa mmoja wa familia yake pana ya Konde Gang.
“Hongera dada mkubwa na shukrani kwa miaka minane ya maisha yako, walinzi bunduki kumbe nalala na wahuni, daah,” Harmonize alimtania Chef Zuwena.
“Zuwena ni Zaidi ya ndugu, shukrani kwa kunilindia tweets zangu. Najua nimekukwaza mara nyingi ila hujawahi nichoka achia mbali ujenzi wa gari unalolipenda ila hii party ni ndogo sijui baby shower ni zawadi nyingine, hongera,” Harmonize aliongeza akisema wanamsubiri malkia mwingine kwenye Konde Gang.
Kwenye ukurasa wa Instagram wa Konde Gang, video nzima ya tukio hilo la kukumbukwa kwa maisha ya Chef Zuwena iliwekwa ikiwaonyesha Harmonize na mpenzi mpya Poshy Queen lakini pia Zuwena wakiwa kwenye picha moja.