Jumamosi mchekeshaji Mulamwah na mpenzi wake Ruth K waliandaa hafla ya babyshower kwa ajili ya mwanao mtarajiwa.
Katika hafla hiyo, Mulamwah alimtiririshia mpenziwe hela nyingi kama njia moja ya kumhongera kwa kumbebea ujauzito.
Mulamwah alipakia video hiyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijami na kusema kwamba ilimlazimu kumimina pesa kwa ajili ya mpenzi wake ili kuonyesha uhalisia wa msimu wa mvua kunyesha.
“Tunakumbatia karatasi … ni msimu wa mvua. Ilikuwa siku njema, hatuwezi kusubiri. Hongera bestie @atruthk kwa baby shower yako,” Mulamwah alisema.
Wawili hao wanafanya babyshower wiki chache tu baada ya kufanya sherehe ya utambulisho wa jinsia ya mwanao.
Walifanya ubunifu wa kipekee ambapo walionekana kwenye maabara wakijifanya watafiti na kudhihirisha kwamba mwanao ajae ni mtoto wa kiume.
Huyo atakuwa mtoto wa kwanza kwa Mulamwah na Ruth K, lakini wa pili kwa mchekeshaji huyo ambaye alipata wa kike na aloyekuwa mpenzi wake, Carrol Sonie.
Licha ya kufahamika mbivu na mbichi kwamba Mulamwah na Ruth K ni wapenzi, bado mchekeshaji huyo ameendelea kumtaja Ruth K kama rafiki yake wa karibu, huku kwa wakati mmoja akifanya mzaha kujitenga na ujauzito huo.
Tazama video hiyo jinsi Ruth K alimiminiwa pesa nyingi;