Msanii wa kike kutoka Pwani, Nyota Ndogo amewakomesha watu katika mitandao ya kijamii wanaomshinikiza kuhusu mimba yake na mpenzi wake mzungu.
Nyota Ndogo ambaye amekuwa akiburuzwa mitandaoni kwa kile baadhi ya watu wanahisi ana mimba ameamua kuvunja kimya chake kuhusu suala hilo na hata kwenda mbali Zaidi kuwatangazia saa na muda kamili mimba hiyo iliingia ili wakapate kujihesabia.
Kwa mujibu wa Nyota Ndogo, alipata ujauzito mwezi Mei mwaka jana, kwa maana kwamba anafaa kutarajia mtoto wake katka kipindi cha chini ya mwezi mmoja lakini ajabu ni kwamba video ambazo amekuwa akipakia katika mitandao ya kijamii zinamuonyesha kwa asilimia kubwa kama mtu ambaye hana ujauzito.
Msanii huyo wa ‘Watu na viatu’ aliwataka wanaomzingua kuhusu mimba kujifanyia hisabati zao wenyewe ili kujua ni lini anafaa kuwa na mtoto, na si kufuatilia mimba yake.
“Sijui tujiachilie ama tusubiri tuzae? Halafu mnani Marakisha kuzaa jamani. Mimba iliingia Mei tarehe 27 saa saba usiku. Hesabuni,” Nyota Ndogo aliwafokea wanamburuza.
Mwaka jana, msanii huyo aliwatambia na kuwavimbia mashabiki wake katika mitandao ya kijamii waliokuwa wanatilia shaka uhusiano wake na mpenzi wake Mzungu mzee.
Nyota Ndogo alipiga picha akionesha kabisa kuwa na mimba, jambo lililowafanya wengi kuhisi kwamba uhusiano wake na Mzungu huyo umekomaa.
Hii ni baada ya kusumbuana na mzungu huyo ambaye alitoroka nchini na kwenda kwao Sweden baada ya Nyota Ndogo awali kumtania kuhusu kuwa na mimba.
Kuondoka kwa mzungu huyo kulimfanya Nyota Ndogo kuhaha kama kichaa, kiasi kwamba aliabiri ndege moja kwa moja kwenye Ulaya kumtafuta mzungu huyo baada ya kudai kwamba alikuwa amemblock kila mahali licha ya kujaribu kumtafuta na hata kuwarai Wakenya kumsaidia kumpata.