Msanii tajiri mmiliki wa lebo ya EMB Records, Kevin Bahati amezua bashasha miongoni mwa mashabiki wake katika mtandao wa Instagram baada ya kupakia picha akiwa na bintiye Mueni ndani ya gari.
Bahati alipakia picha hiyo wakiwa wametabasamu kwa ajili ya picha na binti huyo waliyezaa na mpenzi wake wa kwanza, Yvette Obura na kuwapunga mashabiki wake.
Katika picha hiyo, Bahati alifichua kwamba alikuwa anatekeleza majukumu yake kama baba kwa kumchukua bintiye kutoka shuleni baada ya siku ya masomo kumalizika.
“Majukumu ya Baba 😍 nikimchagua Binti Yangu @Mueni_Bahati kutoka Shuleni ❤️” Bahati aliandika.
Hata hivyo, mashabiki wake idadi kubwa hawakuchelewa kugundua kwamba Bahati na bintiye wanalandana kama riale kwa ya pili na hawakusita kuweka wazi hisia zao hizo.
“Huyu ndio sura yako kabisa 💯” Wanyua12.
“Hii ndio Sura yako sasa 😂😂 na uache filters 🤌” Ryanofficial.0
“Daddy’s photocopy 👏” Lawrence Murage.
“Mueni amefanana na babaa😂” Chunachuna2020.
Wengine pia walifurahia kuona Bahati na bintiye pamoja kwa mara nyingine, baada ya muda mrefu Mueni kukosekana kuonekana katika familia ya Bahati jambo ambalo lilizua maswali mengi kutoka kwa mashabiki wa familia hiyo ya kiceleb.
Baada ya kuona maswali kuhusu kukosekana kwa Mueni katika picha za pamoja za famlia kama awali, Diana Marua aliamua kuvunja ukimya na kuonekana kumtuhumu babymama wa Bahati, Yvette Obura kwa kile alihisi ana roho mbaya.
Akimjibu shabiki wake kipindi hicho Kwa njia ya mafumbo, Marua alidokeza kwamba kutoonekana kwa Mueni pamoja na wenzake chanzo ni mama yake – Yvette Obura. alisema kwamba huenda Obura alilazimika kuondoka na bintiye kutokana na chuki, kutokuwa na shukrani na kutema maneno makali ya matusi.
“Tusimshirikishe Yesu palipo na kutokuwa na shukrani, uchungu na chuki. Upendo na Nuru vitawale,” Diana Marua alijibu.