Kutana na binti mrembo wa Amber Ray na Kennedy Rapudo, apata dili nono la kibiashara (+picha)

Wanandoa hao walisherehekea ukuaji wake mkubwa na kumshukuru kwa kuwa katika maisha yao.

Muhtasari

•Amber Ray na Kennedy Rapudo mnamo Jumanne walifichua uso wa binti yao mrembo, Africanah Ochieng kwa mara ya kwanza.

•Amber Ray kwa upande wake alisherehekea binti yake kwa kupata dili nzuri ya matangazo na duka la urembo la watoto.

Image: INSTAGRAM// KENNEDY RAPUDO

Mwanasholaiti wa Kenya Faith Makau almaarufu Amber Ray na mchumba wake Kennedy Rapudo mnamo siku ya Jumanne walifichua uso wa binti yao mrembo, Africanah Ochieng kwa mara ya kwanza.

Wanandoa hao mashuhuri walimtambulisha binti yao wa miezi minane kwenye mtandao ya kijamii huku wakisherehekea ukuaji wake mkubwa na kumshukuru kwa kuwa katika maisha yao.

"Anapokua, nashuhudia mageuzi ya roho changa inayopitia safari ya maisha. Yeye si tu binti yetu tu; yeye ndiye rubani mwenza wetu katika tukio hili, akitufundisha masomo mazito ya upendo, uthabiti, na dhamana isiyoweza kuvunjika ambayo inatuunganisha pamoja,” Kennedy Rapudo alisema katika taarifa.

Mfanyabiashara huyo tajiri aliambatanisha taarifa yake na picha nzuri zake, mzazi mwenzake Amber Ray na binti yao wa miezi minane.

"Amber Ray umefanya vizuri sana na roho hii nzuri hadi sasa. Hongera sana,” alimsherekea mchumba wake.

Mwanasosholaiti Amber Ray kwa upande wake alisherehekea binti yake kwa kupata dili nzuri ya matangazo na duka la urembo la watoto.

"Uso rasmi wa @enkwanzi_beauty baby products.    Boss baby mwenye umri wa miezi 8. hongera @africanahrapudo," aliandika.

 Amber Ray na mchumba wake Kennedy Rapudo walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza pamoja, Africanah Rapudo mnamo Mei mwaka jana..

 Amber Ray alishiriki habari hizo njema kupitia mitandao ya kijamii akimkaribisha mtoto wake wa pili ulimwenguni.

"Kuhusu msemo 'unaishi mara moja tu" Ninaanza kujiuliza jinsi hiyo ni kweli! Je, inaweza kuwa kweli kwamba siku moja ni kama miaka elfu na miaka elfu kama siku? Ninaweza kuwa na maswali machache zaidi ambayo hayajajibiwa, lakini kwa sasa...

"Mtu wangu yuko pamoja nami kama malaika wa nyumba yangu na mimi ni mama mpya kabisa! Karibu nyumbani mtoto A...nimekuhisi maisha haya yote na sasa naweza kukuona, kukusikia, na kukugusa...NI MAISHA MPYA KABISA 🙌🏾 Maisha ya maisha mengi," Amber Ray aliandika.

Wakati huo huo, Rapudo pia aliweka picha za mpenzi huyo wake akiwa hospitalini baada ya kumkaribisha mtoto wao.