Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee ametangaza ziara ya kikazi nchini Uswizi iliyopangwa kufanyika mwezi ujao.
Siku ya Jumapili, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alishiriki bango lililotangaza kwamba mnamo Machi 2 mwaka huu, atakuwa akitumbuiza katika toleo la sita la Tamasha la Ramogi katika nchi hiyo ambayo ingekuwa nchi ya wakwe zake.
Mama huyo wa watoto watano alieleza zaidi kwamba mpenzi na meneja wake Nelly Oaks ataandamana naye hadi nchi hiyo ya Ulaya.
“Uswisi. Naipendaje hii Ardhi ���������. Kweli, nitakuja na Nelly Oaks wangu kwa taarifa yenu tu ���������. Msiseme sikuwaambia mapema,” Akothee aliandika chini ya bango alilochapisha kwenye mtandao wa Facebook.
Mwimbaji huyo aliendelea zaidi kutangaza upendo wake mkubwa kwa mashabiki wake waUswizi.
Hii itakuwa ziara ya kwanza kwa Akothee nchini Uswizi tangu alipoachana rasmi na aliyekuwa mume wake, Denis ‘Omosh’ Schweizer mwezi Julai. Mwanamuziki huyo na Omosh walikuwa wamepanga kufanya harusi ya pili nchini humo mnamo Julai mwaka jana ila hilo halikutokea, walitengana kabla ya siku kufika.
Akothee alithibitisha kuvunjika kwa ndoa yake na Omosh mnamo mwezi Novemba aliposhiriki kipindi cha moja kwa moja na mashabiki wake kwenye mitandao ya kijamii.
Katika kipindi hicho, mama huyo wa watoto watano alithibitisha kwamba aligura ndoa yake ya muda mfupi mnamo mwezi Juni wakati yeye na Omosh walipokuwa kwenye fungate.
“Nimehama kutoka kwa mahusiano hayo. Hayapo tena. Ninataka kuwaaambia kwamba nilitoka kwenye uhusiano huo mwezi Juni. Hata hivyo sitaeleza kwa undani,” Akothee alisema.
Aliongeza, “Nilifurahia ndoa yangu, nilifurahia harusi yangu. Sijutii chochote. Nilifanya harusi yangu mnamo siku ya kuzaliwa kwangu ndio ikiwa tu mambo yangeenda vibaya, kama wamefanya, basi singekuwa na majuto yoyote.”
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alidokeza kwamba aligura ndoa yake baada ya kujifunza mambo kadhaa ambayo hakujua hapo awali.
Hata hivyo alidokeza kwamba hakumwambia mzungu huyo kutoka Uswizi kuhusu uamuzi wake mara moja na hata walipokuwa wakiagana, alimdanganya kwamba hangemuacha.
"Nilitoka nje ya uhusiano mnamo Juni. Kawaida mimi hutoka nje ya uhusiano wangu wakati bado niko kwenye uhusiano. Tulipokuwa kwenye fungate, niligundua mambo fulani ambayo sikuweza kustahimili. Kisha akaniuliza, “Utaniacha?” Nikasema, "hapana mpenzi nakupenda". Nilipokuwa nikitoka Uswizi mnamo Julai, kwenye uwanja wa ndege aliniuliza," utaniacha?, Nikasema "hapana mpenzi, nakupenda". Lakini kwa hakika, nilikuwa tayari nimeondoka,” Akothee alisimulia