logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Niko na stress, sitaki kutafutwa!" Jumbe za kutisha za msanii Masauti zazua wasiwasi

Msanii asauti ameibua wasiwasi miongoni mwa mashabiki wake baada ya kuandika jumbe za kutatanisha kwenye Instagram.

image
na Samuel Maina

Burudani09 February 2024 - 05:10

Muhtasari


  • •Msanii asauti ameibua wasiwasi miongoni mwa mashabiki wake baada ya kuandika jumbe za kutatanisha kwenye Instagram.
  • •“Niko na stress, sitaki kutafutwa. Akili yangu imechoka tafadhalini,” alisema.

Mwimbaji mashuhuri wa Kenya mzaliwa wa Pwani, Mohammed Ali Said almaarufu Masauti ameibua wasiwasi miongoni mwa wanamitandao na mashabiki wake baada ya kuweka jumbe za kutatanisha kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram.

Mwimbaji huyo ambaye anafahamika kwa sauti yake nzuri ya muziki alichapisha machapisho kadhaa siku ya Alhamisi akidokeza kuwa hayuko sawa.

Katika chapisho lake la kwanza, alichapisha video iliyomuonyesga akifurahia kinywaji na baadhi ya marafiki zake na chini ya video hiyo, akabainisha kuwa atakuwa sawa.

“Niko sawa, lakini siko sawa, lakini nitakuwa sawa Inshallah, Amin,” Masauti aliandika.

Katika chapisho lingine, mwanamuziki huyo mzaliwa wa pwani alidokeza kuwa anapambana na msongo wa mawazo. Kuongeza wasiwasi, alidokeza kuwa hataki kusumbuliwa.

“Niko na stress, sitaki kutafutwa. Akili yangu imechoka tafadhalini,” alisema.

Pia aliweka chapisho lingine akiomba Mungu aingilie kati na kumwokoa kutoka kwenye shida aliyonayo ambayo hakutoa maelezo zaidi juu yake.

“Allah najua unaniona kijana wako siko sawa. Nipee nguvu nishinde hii changamoto,” alisema.

Mwaka jana, Masauti alifichua kuwa yeye ni mtu aliyeacha shule. Alieleza kushangazwa kwake na kujiunga na shule ya upili akizingatia matokeo yake duni katika KCPE.

'Dah' alimwambia Obinna, akionyesha kuwa alianguka.

Alisoma katika shule nyingi, akitaja angalau taasisi tatu tofauti. Mzaliwa huyo wa Mombasa alimweleza Oga Obinna katika mahojiano kuwa aligundua safari yake ilikuwa ya muziki.

"Ah noma," aliongeza, "Noma ipepete, ilinipepeta yani ni kusema ukweli wacha nikuwe honest, hata mtu akiniona asiniulize maswali ama vipi," alisema.

Alisema kuwa alifanya vibaya na elimu haikuwa jambo alilopenda kufanya

"Bwana sikuwa vizuri, sikuwa vizuri kabisaaaa kabisa. So at least nikafika hapo form mbili, nikaachilia hapo lakini results za Class 8 hazikuwa vizuri.

Ni ile tuu niliskuma skuma mpaka form two lakini niliona hata sijui nilifika aje form two. Ilikuwa noma, hapo form one sikuwahi kusoma hata nikashangaa niko form two hio form one hata sijui nilipita aje.

Lakini Alhamdulilahi, Mungu ni nani akikunyima hapa anakupatia huku akasema kijana wangu we ni mwimbaji si msomi fanya uimbaji wako bora tuu utie bidii."

Pia alisema kwamba aliacha shule kwa sababu nyingine, "Sikuwa na pesa." Anamshukuru Mungu kwa mafanikio ya muziki licha ya kufeli shuleni.

Masauti ameshirikiana na wanamuziki kadhaa mashuhuri nchini wakiwemo Mr. Seed, Nadia Mukami, na Khaligraph Jones nk.

Katika mahojiano, alifichua kuwa yuko kwenye mahusiano, na wamekuwa pamoja na mpenziwe kwa muda. Anapendelea kuweka habari kuhusu utambulisho wake siri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved