Wako wapi sahi? Fahamu waliko sasa waliokuwa wanamuziki tajika

Wengine wamesahulika hata baada ya kutoa ngoma kali kal

Muhtasari
  • C-zars ni mwanamziki anaye julikana kwa wimbo wake "Amka Ukatike" ambayo ulimletea umaarufu.
  • Baada ya kutoa albamu yao ya " Many faces" walizunguka Amerikani  na Europa na tangu wakati huo, kikundi hiyo hawajaskika tena kando ya maonyesho yao ya  mara kwa mara.

Katika miaka michache iliyopita, tumepata kuona wanamuziki hodari ambao kwa sasa wametoweka kwenye tasnia.

Wengine wamesahulika hata baada ya kutoa ngoma kali kali.

Tutaangalia baadhi ya wanamuziki hao.

1. C-zars

C-zars ni mwanamuziki anaye julikana kwa wimbo wake "Amka Ukatike" ambao ulimletea umaarufu.

Akiwa miaka 17, C-zars tayari alikuwa kwenye vichwa vya habari vya muziki wake.

C-zars alitoweka mwaka 2006, wiki moja baada ya kukalia mtihani wake wa KCSE. Hajulikani alikoenda.

Katika mahojiano na mwanahabari  John Muchiri, Mzee Makasi, babake C'zars alisema kuwa umaarufu huo wote iliingia kichwani cha mwanake mwake mpaka ilifika hatua akamfunga Mombasa kituo cha polisi kwa utoro.

Mzee Makasi aliendelea na kueleza kuwa hakuna mwanamuziki aliyetaka kufanya kazi na kijana wake kwa sababu walihisi kutishiwa na talanta ya kijana wake. 

"No musician liked him out here in Mombasa, it was very evident. They all felt threatened by his instant success," babake alisema. 

Anaamini kuwa kuna baadhi ya sababu zingine ambazo zilisababisha kutoweka kwa mtoto wake. 

“Even after all those painful days, I am still hopeful and waiting patiently. Either he shows up or at least I get to know what happened to him,” 

Hata baada ya siku hizo za uchungu, nina imani na kusibiri kwa subira kuwa arudi nyumbani ama nijue kitu ambalo kilimfanyikia", Mzee Makasi alisema.

2. GidiGidi- MajiMaji

Baada ya kutoa albamu yao ya " Many faces" walizunguka Amerikani  na Europa na tangu wakati huo, kikundi hicho hakijafanya muziki pamoja kando ya shoo zao za  mara kwa mara.

Wanajulika kwa wimbo wao wa "Atoti" na " Unbwogable".

GidiGidiMajiMaji

GidiGidi MajiMaji  ni waimbaji wa hiphop ambao yimbo zao nyingi ziko katika lugha ya Kijaluo, pamoja na Kiingereza na Kiswahili. Tofauti na wasanii wengi wa hip hop nchini, GidiGidi MajiMaji huchanganya kwa hiari midundo ya Kiafrika na muziki wao.

MajiMaji ambaye anajulikana pia kama Julius Owino ni Mkurungenzi mtendaji wa kituo kimoja cha redio cha humu nchini na amekua kwa nafsi hiyo tangu Februari 14 2014 mpaka wakati huu.

GidiGidi ni mtangazaji wa kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kwenye Radio Jambo.

Majimaji pia ametoa wimbo na mwanamziki anayejulikana kama  Blinky Bill. Blinky alimshirikisha majimaji kwa wimbo wake wa Boss kwa albamu wake wa "We Cut Keys 2".

3. Elani

Elani ni kundi ambalo linajumuisha Maureen Kunga, Wambui Ngungi na Bryan Chweya. Hao wote kwa sasa wanafanya miradi yao wenyewe. 

Bryan Chweya, mmoja wa kikundi hilo alizungumza baada ya watu kulalamika kuwa wamenyamaza sana na hawako pamoja, akieleza kuwa hakuna siku hajawahi kuwa pamoja.

Wametoa albamu kadhaa kama Barua ya Dunia, Seven Places, Elani Instrumentals, Colours Of Love na Speaking in Cursive.


Elani
Image: Instagram

Aliendelea na kusema kuwa hata Nyashinski alipumzika kwa miaka kumi na bado alirudia mziki.

" We have many projects that we are working on and regardless of guys complaining that we have been silent for long, there is no day that Elani will not be together". " For example rapper Nyashinski went on more than a 10 year hiatus and he came back with  one big song  and it was like he never left", Bryan alieleza.

Wambui naye alieleza kuwa  ni lazima kila mtu apewe fursa ya kukua.

"What we have understood as a group is that it is important, especially if you exist in a music group to give each member an opportunity to explore their other gifts" 

4. Camp Mulla

Licha ya mafanikio yao, walitangaza kuwa hawatukua wanatoa mziki tena pamoja mwaka wa 2013.

Mwaka wa 2013, Camp mulla walitoa wimbo wao wa kwanza "Party don't stop" kutoka albamu yao ya "Funky Town" na hiyo ndio albamu pekee walitoa kama kikundi.

Baada ya mgawanyiko yao, walipatana tena kwenye tamasha mwaka wa 2017 na mashabiki wao walijawa na furaha kwa kuwa walikua wanadhania wamerudi kutoa mziki pamoja.

Anayejulikana zaidi kutoka kikundi hicho ni Miss Karuna ambaye sai anafanya mziki pekee yake na anafanya vizuri sana.