DJ Pierra Makena afichua kwa nini bado hajaolewa akiwa na miaka 42

Alifichua kuwa sababu yake ya kutoolewa ni kuwa hajapata mwanaume sahihi kwake.

Muhtasari
  • Alifichua kuwa alipata mtoto wake wa kwanza Ricca Pokot akiwa miaka wa 35 na sai ako 42. 
  • "Watoto wenzake walikuwa wanamuuliza babake ako wapi na hii ilifanya nitafute babake ili niwaunganisha tena lakini haikufaulu," alisema.
Dj Pierra Makena/Instagram
Dj Pierra Makena/Instagram

Mwigizaji na Dj wa Kenya Pierra Makena amefunguka kuhusu kwa nini bado hajaolewa ilhali ako na umri wa miaka 42.

Katika mahojiano na Oga Obinna, alifichua kuwa sababu yake ya kutoolewa ni kuwa hajapata mwanaume sahihi kwake.

Mama huyo wa mtoto mmoja aliendelea kulalamika kuwa kuna wanawake amabo wanamkosoa kwa sababu hajaolewa bado.

"Sipendi wanawake wakikashifu wanawake wengine kwa sababu hawajolewa. Kuna wengine huniambia ati naongea vile naongea kwa sababu sijaolewa".

" Sitaki kuwa mwanamke ambaye anaolewa na mtu mbaya kwa sababu nataka kufurahisha jamii. Sijaolewa kwa sababu sijapata mwanaume anayenifaa bado"

Alifichua kuwa alipata mtoto wake wa kwanza Ricca Pokot akiwa miaka wa 35 na sai ako 42. 

Aliendelea kusema kuwa mtoto wake alikuwa anapitia matatizo mbalimbali akiwa shuleni na hiyo ilimlazimisha kumtafuta baba ya mtoto ili wajuane zaidi lakini haikufaulu.

" Mtoto wangu alikua anapitia mengi sana sana shuleni. Watoto wenzake walikuwa wanamuuliza babake ako wapi na hii ilifanya nitafute babake ili niwaunganisha tena lakini haikufaulu". Watakapokuwa tayari kuunganishwa tena, ntawapa huo nafasi", Pierra Makena alisema.

Aliendeleza na kusema, " Mimi siwezi  kuzungumza vibaya kuhusu baba  wa mtoto kwa mtoto wangu na pia siwezi peleka mwanaume kortini ndio anipee pesa badala yake, naweza mpeleka korti kumpenda mtoto wake."

Alijulisha watu kuwa anasherekea miaka 15 kama DJ na hiyo ndio kazi pekee anafanya kwa sasa juu aliacha kazi ya siku.