Rapa mwenye misemo ya kuchekesha kutoka Kibera, Stevo Simple Boy kwa mara nyingine ametoa tahadhari nzito kwa wanaume wenzake kwamba warembo wao wanashinda wakimsumbua katika DM zake.
Kupitia Instagram yake, Stevo Simple Boy alichapisha picha yake akiwa amevalia nadhifu kuanzia durag kwenye kichwa na shati jekundu huku akimwaya tabasamu na kujisifia kwamba yeye ni mwanaume mtanashati Zaidi ambaye vipusa wengi wanamfuata kwenye DM zake.
Msanii huyo wa Freshi Barida aliweka wazi kwamba warembo hao licha ya kuwa na wapenzi wao, wanashinda wakimsumbua kwa ombi la kutaka kuolewa na yeye, akifichua kwamba kinachomponza ni utanashati wake.
“Ooo mara Stevo I want to marry you...ma girlfriend's wenu wananisumbua sikupenda Kwangu mimi kuwa hensam boy...,” Stevo alisema.
Mashabiki wake hawakuchelea kumtania kwa tamko hilo, wengine wakimsifia na wengine wakimsimanga kwa viwango sawa.
“Wewe ni msanii ninayempenda sana wa vietinam katika globu hii 2024, mambo lombolombo Mr verses!” mmoja alisema.
“Wewe si simple boy,wewe ni real boy” Wanawaweru alisema.
“Wewe sio mrembo tu bali ni mcheshi🤪🤪 vile vile 😅😅😅.” Just tina85 alisema.
Msanii huyo amekuwa akizungumziwa katika siku za hivi karibuni haswa baada ya kudai kwamba akiwa mdogo aliwahi fariki dunia na kisha kufufuka baada ya muda mfupi.
Katika mahojiano na Trudy Kitui, Stevo aliweka wazi kwamba maisha yake ya utotoni yalikuwa na changamoto si haba, kwani aliwahi kuwa mgonjwa na mamake akamkimbiza hospitalini ambapo alifariki na kwa neema ya Mungu akapata ufufuo.