Mbunge wa Mumias Peter Salasya amjibu Pierra Makena kuhusu madaiwa ya kummezea mate kisirisiri

" Tutaona jinsi mambo itaenda, mambo ni pole pole".

Muhtasari
  • Katika mahojiano na wanayoutube, Salasya alisema kuwa hajui amekutana na Pierra mara moja na ako tayari kukutana na yeye mara nyingine.
Peter Salasya na Pierra Makena

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya amemjibu Dj Pierra Makena ambaye katika mahojiano yake na Oga Obinna alifichua kuwa anamezea Salasya mate.

Katika mahojiano na wanayoutube, Salasya alisema amekutana na Pierra mara moja na ako tayari kukutana na yeye mara nyingine.

"Watu wanaponipenda huwa najiskia raha sana, mwambie tu mimi pia namtafuta na anitafute tutaftane. Nimemuona kwa mara ya kwanza lakini  mtaniambia siku anakuwanga na show ili niende nione show yake inakuwanga aje. Anachezanga reggae ama anachezanga ngoma gani?"

Wanayoutube hao walipojulisha kuwa yeye ni deejay na ancheza muziki wa aina  zote, Salasya alisema;

" Mwambie tu nitakuja kwa gig yake". 

Waliendelea kumuuliza kama anaweza penda kukuwa na uhusiano wa mapenzi na deejay huyo alisema kuwa,

" Tutaona jinsi mambo itaenda, mambo ni pole pole".

Waliendelea kumuuliza kuhusu maoni yake juu ya mtayarishaji wa maudhui Kaspul aliyesema sema kuwa yeye bado ni kijana mdogo sana na aachane na Pierra. Mbunge huyo wa Mumias mashariki alisema , " Sasa si dem anapenda yule mwenye anataka".