Tumepata kuona watu mashuhuri kutoka nchi ya Kenya wakizamia masuala ya kisiasa ili waweze kutumikia wananchi katika nyadhifa mbali mbali.
Leo tutakuwa tunaangazia baadhi ya watu hao ambao wameonyesha ari ya kuijunga na siasa au tarayi eazamia katika siasa.
1. Mc Jessy
Mchekeshaji Mc Jessy ambaye jina lake halisi ni Jasper Muthomi, alitangaza rasmi kuwa atagombea kiti cha Ubunge wa Imenti kusini wakati wa uchaguzi wa August 9 mwaka wa 2022.
2. Eric Omondi
Mcheshi na mwanaharakati Erick Omondi Katika mahojiano na kituo cha redio cha ndani alifichua kuwa angetaka kugombea kiti cha ubunge cha Lang'ata.
Aliendeleza kuwa ni wakenya ndiyo wanataka agombee kiti hicho lakini bado hana uhakika.
3. Jalang'o
Mtangazaji wa zamani wa redio Phelix Odiwuor almarufu Jalong'o alitangaza kuwa atawania kiti cha langata mnamo 2022 ambacho alishinda na ndiye mbunge wa hivi karibuni wa Langa'ta.
4. Cassypool
Muundaji wa maudhui Cassypool mwaka jana alifichua kuwa rais baada ya rais William Ruto.
Mwaka huu ameeleza kuwa anataka kugombea kiti cha ugavana wa Nairobi mgombea mwenza wake akiwa Neema Abdikadir almarufu Nimoreee aliyekuwa kiongozi wa wanafunzi.
5. Jaguar
Mwanamuziki wa Kenya Jaguar ambaye jina lake halisi ni Charles Njagua Kanyi, aligombea kiti cha ubunge cha starehe mnamo 2017 na alishinda. Mwaka jana aliteuliwa CAS (Chief Administrative Secretary) na rais William Ruto.
6. Jamal Gadafi
Mtangazaji wa zamani wa runinga Jamal Gaddafi ni miongoni mwa wagombea sita waliotangaza nia ya kiti cha ubunge cha Malindi wakati wa uchaguzi wa mwaka 2022, 9 August.
7. John Kiarie Waweru
Kj anavyojulikana ni mcheshi wa zamani wa kikundi cha Redkyulass. Kj yeye ni mbunge wa Jimbo la Dagoretti Kusini.
8. Johnson Sakaja
Johnson Sakaja ambaye ni gavana wa Nairobi county pia alifichua kuwa kabla ya kuingia katika siasa alikuwa msani anaye rap.
9. Sabina chege
Sabina Wanjiru Chege kabla ya kuingia katika siasa alikuwa mtangazaji wa redio na mwigizaji wa televisheni. Alikuwa mwakilishi wa wanawake mwaka wa 2013 na 2017 katika uchaguzi mkuu.
10. Proffesor Hamo
Mcheshi Herman Gakobo Kago almarufu Professor Hamo anatazamia kiti huko Nakuru Mashariki.
11. Alex Mwakideu
Mtangazaji wa redio Alex Mwakideu alitangaza kugombea kiti cha kisiasa mnamo 2022. Alisema atauwania kiti cha ubunge cha Wundanyi.