TikToker Kelvin Kinuthia ameamua kuweka kero lake wazi kwa baadhi ya mashabiki wake wanaokutana naye hadharani na kumsalimia kama mwanamume.
Mkuza maudhui huyo wa kiume anayevaa mavazi ya kike na kutumia vipodozi kama mwanamke katika video yake ya hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii alisema kwamba kuanzia sasa kwenda mbele, hatoweza kumtambua mtu yeyote ambaye atamsalimia kama ‘kaka’.
Kinuthia alisema kwamba anagharamika pakubwa kwa mavazi ya kike pamoja na vipodozi ili kuonekana kama mwanamke lakini baadhi ya watu bado wakikutana naye wanamsalimia, ‘niaje bro’ – jambo ambalo humkera sana.
“Hapana, hapana, hapana rafiki zangu, mimi kuna kitu kimenikasirisha. Yaani tunakutana na wewe kwa Mall ama tuseme kwa Supermarket. Na huu urembo wote, na hizi kucha zote, unaniambia ‘niaje bro?’… kwanza tuanzie hapo, kaka yako ni nani?” Kinuthia aliuliza.
Jamaa huyo ambaye hajawahi weka wazi msimamo wake katika suala la utambulisho wa jinsia pia alitoa kero lingine ni lile la kusalimiwa kwa salamu za kugongana kwa mabega – salamu aghalabu zinazohusishwa na wanaume wawili wakikutana.
Aliwataka watu wanaotaka kumsalimia kumtambua kama ‘baby girl’ la sivyo wakae na salamu zao.
“Ama mtu unanikujia na salamu za kugongana hapa kwa mabega, aaaagh na ukinivunja mabega? Mimi kama huwezi nisalimia na mkono ama huwezi nipa hug, salamu zako ukae nazo. Na kama unajua utaniambia ‘niaje bro’ sitaki. Kama huwezi niita ‘baby girl’ tafadhali kaa na salamu zako,” alimaliza.
Hii hapa video ya Kinuthia akitoa onyo hilo kali;