logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ikitokea Wema Sepetu ameniacha najitupa baharini nife - Whozu atishia (video)

Wawili hao wamekuwa pamoja kimapenzi tangu 2022.

image
na Davis Ojiambo

Burudani28 February 2024 - 11:19

Muhtasari


  • • Penzi la wawili hao limekuwa likikosolewa pakubwa kutokana na utofauti mkubwa wa umri baina yao.

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Whozu amefunguka kitakachotokea kwa maisha yake endapo mpenzi wake Wema Sepetu atafanya uamuzi wa kumuacha

Akizungumza kwenye kituo cha redio cha East Africa, Whozu alisema kwamba endapo Wema Sepetu amemuacha leo hii, atafululiza moja kwa moja hadi baharini na kujitosa majini na kufia huko.

Whozu alikuwa akiwajibu wanaomuuliza cha kufanya iwapo Wema atamuacha – jambo ambalo wengi wanaona litatokea hivi karibuni.

“Endapo mama [Wema Sepetu] ameniacha kwa kweli, dah, mimi nitajitupa baharini, mazishi Moshi na mje. Si vibaya kumpenda mtu, unajua ukipendwa kubali na appreciate, usijifanye. Muonyeshe kama unampenda, onyesha usifiche.”

“Mimi niko radhi kupigana na mtu yeyote kwa ajili ya mwanamke wangu, kwa sababu nampenda. Kwa hiyo msimuongelelee vibaya, msiseme kitu chochote cha kunikwaza. Mtu yeyote, si ndugu, sio wazazi, siingiliwi kwenye suala langu. Mtu yeyote yule hatakiwi kuingilia katika suala langu la mapenzi,” alisema.

Katika mahojiano mengine wiki chache zilizopita, Whozu alifichua kwamba yeye ndiye anaendesha akaunti zote za mitandao za Wema Sepetu.

Msanii huyo wa ‘Ameyatimba’ alisema kwamab wanaume wote wanaomtongoza Wema kwenye DM majibu wanayoyapata ni yeye anawajibu wala si Wema Sepetu.

Penzi la wawili hao limekuwa likikosolewa pakubwa kutokana na utofauti mkubwa wa umri baina yao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved