Siku chache baada ya Zari kuthibitisha kuwepo kwa nyufa kubwa katika penzi lao na mumewe Shakib Cham, mapya yameibuka kuhusu maisha mapya ya kijana huyo.
Shakib ambaye ni mdogo kiumri kwa Zari kwa muda amekuwa akisemekana kutokuwa na kitu chochote cha kumuingizia pesa, Zaidi ya kuwa katika mapenzi na Zari tu.
Sasa baada ya Zari kufichua kwamba Shakib alifungasha virago na kuondoka nyumbani, imebainika kwamba kijana huyo ameanza kutafuta riziki yake kwa kuwalipisha wanablogu wanaotaka kumuuliza kitu chochote kuhusu ndoa yake.
Katika screenshot moja ambayo imekuwa ikienezwa mitandaoni, Mange Kimambi kutoka Tanzania alimfuata Shakib kwenye DM ya Instagram na kuomba kufanya mazungumzo na yeye kuhusu tukio zima linaloendelea baina yake na Zari lakini pia na video yake na Diamond.
Shakib kabla ya kumjibu Mange alisema kwamba hapendi kufanya mahojiano lakini iwapo anataka kumhoji, basi akubali kwanza kumlipa.
Katika mazungumzo hayo, Shakib alitaka kutumiwa kiasi cha dola elfu moja, sawa na shilingi za Kenya 147,000 kabla ya kuulizwa swali lolote.
Zari hata hivyo hakufurahishwa na hulka hiyo mpya ya Shakib na alimkasirikia Kimambi kwa kutaka kumrubuni Shakib kwa ajili ya kupata taarifa za ndani kumhusu.
Maoni ya Zari yanakuja moto baada ya Mange Kimambi kuwaalika wafuasi wake kutazama mahojiano hayo yenye utata na Shakib, hatua iliyozidisha mvutano kati ya pande zinazohusika.
“Ohh simpendi bi tuks lakini ulilipa $1000 nzima kwa mtu kukupa umbea kunihusu. Niambie wewe ni shabiki wangu mmoja, bila kuniambia kuwa unanihusu sana. Kwa hivyo nimewekeza katika maisha yangu.”
“Kwa utundu huo unaweza kuua mtu hapa ndio sehemu nzuri hata baada ya kuedit ulitoka huna kitu alishindwa kukupa ulichotaka baby nitumie waridi na pesa hizo.Kama nionyeshe nakupenda bila kuniambia unanipenda alikuwa mtu,” Zari Hassan alisema kupitia insta story yake.