logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mimi ni female version ya Samidoh katika mapenzi – Manzi wa Kibera

"Kila mtu anakaa huko kivyake, ni mimi tu kuzunguka kutoka kwa mmoja kuelekea kwa mwingine."

image
na Davis Ojiambo

Burudani29 February 2024 - 09:08

Muhtasari


  • • Alisema kwamba sawa tu na Samidoh anayefanya mizunguko kutoka kwa Karen kwenda kwa Edday Marekani na kurudi, naye anatoka kwa Nzioki kwenda kwa Njau.
Manzi wa Kibera ajifanaisha na Samidoh katika mapenzi

Manzi wa Kibera amefunguka kuiga nyayo ya msanii Samidoh katika suala zima la mapenzi baina ya wanawake wake wawili.

Mrembo huyo amefichua hayo baada ya kudai kwamba amerudiana na Nzioki, mpenzi wake mwenye umri wa miaka 67.

Hata hivyo, Manzi wa Kibera aliweka wazi kwamba licha ya kurudiana na Nzioki, bado hajaachana na Daniel Njau, mzee mwingine mwenye umri wa miaka 75.

Alisema kwamba atachumbiana na wazee wake wote kwa wakati mmoja kama ambavyo Samidoh anafanya kwa Karen Nyamu na Edday – kila mmoja akiwa na wakati wake na mgao wa penzi pia kwa usanjari.

“Wewe ushawahi ona Karen [Nyamu] na Edday] Nderitu] wakipatana? Mimi ndio female version wa Samidoh. Hawa watu hawawezi kutana, kwa sababu wakikutana itakuwa ni vita nyingine ya dunia. Kila mtu anakaa huko kivyake, ni mimi tu kuzunguka kutoka kwa mmoja kuelekea kwa mwingine. Shughuli kibao,” Manzi wa Kibera alifichua mpango wake na wazee wake.

Alisema kwamba sawa tu na Samidoh anayefanya mizunguko kutoka kwa Karen kwenda kwa Edday Marekani na kurudi, naye vile vile amechukua mkakati kabambe kuhakikisha wazee wake wote hawakutani, kama njia moja ya kulinda amani ya penzi lake kwao.

“Hawajawahi patana. Kila mtu anacheza kivyake. Naweka mitandaoni lakini hakuna mtu ako na simu, niliwanyang’anya wote ndio uwanja uwe safi. Nachumbiana na wao kwa wakati mmoja, hakuna siku nilijitokeza na kusema nimmeachana na Nzioki [mzee wa miaka 67].”

“Ni kama Samidoh ambaye hajawahi kuja kutuambia kwamba yeye na Karen wamewahi pigana. Hapana! Ako na Karen, ako na Edday. Akiamka asubuhi aende USA arudi kesho jioni alale Runda hakuna mtu atamuuliza kwa sababu hajawahi sema wameachana. Huyo ndio mimi sasa, sijawahi achana na  Njau na sijawahi achana na Nzioki, nina wote; mume wangu Nzioki, mume wangu Njau!” alimaliza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved