logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa shoga alia na kuvuruga harusi ya mumewe baada ya kugundua anaoa mwanamke (Video)

Juhudi za kumtuliza zilifeli na aliapa kuvuruga harusi hiyo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani02 March 2024 - 09:06

Muhtasari


  • • Kulingana na ripoti, shoga huyo na mpenzi wake walikuwa wamechumbiana kwa zaidi ya miaka 5 na kutupwa kwa mwanamke mwingine.
Mwanamume shoga avuruga harusi ya mpenziwe

Kizaazaa kilishuhudiwa katika kanisa moja nchini Afrika Kusini baada ya mwanamume shoga kuvuruga harusi akidai kwamba mwanamume aliyekuwa anafunga harusi na mrembo wake ni mpenzi wake.

Katika video fupi kutoka kwa tukio hilo, mwanamume huyo shoga alifika wakati mwafaka kabla ya mhubiri kuwashikanisha mke na mume kuwa kitu kimoja na kuzua rabsha, asiweze kutulizwa na mtu yeyote.

Jamaa huyo aliyekula na kusitunya alionekana akijitupa sakafuni na kujigaragaza kwa hasira akiteta kwamba mpenzi wake – mwanamume – alikuwa ameratibu harusi yake kinyemela licha ya kujua kwamba walikuwa katika uhusiano wa kishoga.

Kulingana na ripoti, shoga huyo na mpenzi wake walikuwa wamechumbiana kwa zaidi ya miaka 5 na kutupwa kwa mwanamke mwingine.

Licha ya mashuhuda wa tukio hilo kujaribu kumtuliza, bado alipiga kelele na kuapa kuharibu tukio zima.

Tazama video hapa chini kujua zaidi...


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved