logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mke atoroka ndoa kwa kugundua mumewe amekuwa akila placenta za wanawe 3 (video)

Baadhi walikiri kwamba kuna koo fulani wanakula placenta.

image
na Davis Ojiambo

Burudani08 March 2024 - 08:41

Muhtasari


  • • Siri ya mumewe ilifichuka baada ya kutumwa nje ya hospitali kwenda kuchukua dawa kwenye duka la dawa baada ya mkewe kujifungua mtoto wa tatu.
  • • Kwa kawaida, mume huhakikisha kwamba kiungo hicho kimetengwa ili apeleke nyumbani lakini kwa kuwa hakuwepo, hospitali ilikitupa.
Mke agura ndoa mume akila placenta

Mama mwenye watoto watatu ameitoroka ndoa yake na anatathmini kuomba talaka yake rasmi baada ya kugundua tabia isyo ya kawaida kutoka kwa mumewe.

Kwa mujibu wa jirani wa wanandoa hao ambaye aliipeleka simulizi yao kwenye TikTok, alieleza kwamba mama huyo jirani aligundua mume wake amekuwa na hulka ya kula placenta za wanawe pindi wanapozaliwa.

Mama huyo aligundua hili baada ya kujifungua mtoto wa tatu hospitalini pasipo na mumewe, ambaye alifika na kutaka kupewa placenta lakini akaambiwa alichelewa na hivyo ikatupwa.

Siri ya mumewe ilifichuka baada ya kutumwa nje ya hospitali kwenda kuchukua dawa kwenye duka la dawa baada ya mkewe kujifungua mtoto wa tatu.

Kwa kawaida, mume huhakikisha kwamba kiungo hicho kimetengwa ili apeleke nyumbani lakini kwa kuwa hakuwepo, hospitali ilikitupa.

Mara baada ya kugundua placenta limekwisha tupwa, alisababisha tukio hospitalini lakini tayari walikuwa wamechelewa na walikuwa wamelitupa.

Mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini, kila kitu nyumbani kwao kilianza kwenda kando.

Hapo ndipo mume alipokiri kwamba ni kwa sababu hakula placenta la mtoto wa mwisho kama ilivyo desturi katika mji wake.

Ufichuzi huo ulizua hofu kwa mwanamke huyo alipokuwa akipakia vitu vyake na kuondoka katika nyumba ya mumewe.

Ni vyema kutambua kwamba placenta ni chombo kinachoendelea katika tumbo la mama wakati wa ujauzito. Muundo huu hutoa oksijeni na virutubisho kwa mtoto anayekua. Pia huondoa bidhaa za taka kutoka kwa damu ya mtoto. Watoto wengi huzaliwa na placenta.

Video hiyo iliibua hisia kinzani, wengine wakisema kwamba katika tamaduni zao, ni shrti mtu baada ya kujifungua arudi nyumbani na mtoto lakini pia na placenta kwa ajili ya kuzikwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved