Shakib amfichua mama mkwe mrembo wa Zari, aonyesha kumbukumbu yao nzuri

Mumewe Zari alimsherehekea mama yake wakati ulimwengu mzima ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Muhtasari

•Shakib alishiriki video nzuri ya kumbukumbu yake na mamake katika hoteli ya kifahari ambapo alikuwa amempeleka mzazi huyo kwa likizo.

•Pia alitumia Siku ya Kimataifa ya Wanawake kumsherehekea mkeee Zari na kumhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

Zari Hassan, Shakib Cham, na mamake Shakib
Image: INSTAGRAM// SHAKIB CHAM

Siku ya Ijumaa, mfanyibiashara wa Uganda Shakib Cham Lutaaya alimsherehekea mama yake wakati ulimwengu mzima ukiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Mume huyo wa mwanasosholaiti Zari Hassan alishiriki video nzuri ya kumbukumbu yake na mama yake katika hoteli ya kifahari ambapo alikuwa amempeleka mzazi huyo kwa likizo.

Katika sehemu ya maelezo ya video hiyo aliyochapisha kwenye mtandao wa Instagram, Shakib alimsherehekea mzazi huyo wake na kutumia fursa hiyo kumhakikishia kuhusu  upendo wake mkubwa kwake.

"Kheri ya siku ya kuzaliwa Hajat.. Nakupenda," Shakib aliandika chini ya video hiyo ya kupendeza.

Hajat katika Uislamu maana yake ni "kutamani."

Katika picha hiyo, mamake Shakib alionekana akiwa amevalia mavazi mekundu na alionekana kufurahishwa sana na likizo hiyo. Alionekana mwenye afya njema na mwenye nguvu.

Mfanyibiashara huyo wa Uganda pia alitumia Siku ya Kimataifa ya Wanawake kumsherehekea mke wake Zari Hassan na kumhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake.

"Kheri ya Siku ya kuzaliwa mpenzi, wewe ni mzuri.. Nakupenda mama @zarithebosslady," Shakib aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha za hivi majuzi zake na mama huyo wa watoto watano wakifurahia wakati pamoja katika nchi ya jangwa ya Dubai.

Hivi majuzi wanandoa hao walithibitisha kurudiana kwao, wiki chache tu baada ya kudokeza kuhusu matatizo ya ndoa ambayo yalidaiwa kufanya watengane.

Wanandoa hao walithibitisha kurudiana kwao siku ya Jumatano waliposhiriki picha zao nzuri wakiwa pamoja kwenye sherehe za Umrah 2024 nchini Saudi Arabia.

Shakib alichapisha picha na video nzuri zake na mkewe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuziambatanisha na jumbe za kupendeza na emoji za mapenzi.

"Chini ya kijani ni mahali ambapo nabii wetu mpendwa alizikwa," Shakib aliandika chini ya moja ya video alizochapisha.

Video na picha zingine ambazo kijana huyo wa miaka 32 alichapisha zilimuonyesha yeye na mkewe wakizunguka katika mji mzuri wa Riyadh nchini Saudi Arabia.

Zari pia alishiriki baadhi ya video na picha za ziara yao katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.