Mwanasosholaiti mashuhuri wa Uganda na mfanyibiashara Zari Hassan ameweka wazi kuwa hahitaji ushauri kutoka kwa watu wa nje kuhusiana na uamuzi wake wa kurudiana na mume wake, Shakib Cham Lutaaya siku kadhaa zilizopita.
Huku akiwajibu wanamitanda ambao wameonyesha kutaka kuingilia mambo yake ya kibinafsi kupitia video kwenye akaunti yake ya snapchat, mama huyo wa watoto watano alionyesha kutopendezwa na maoni na ukosoaji kutoka kwa wale ambao hawakuaombwa ushauri ama kuchangia.
"Ukija hapa na maoni yako na senti zako mbili na hakuna mtu aliyekuuliza, sitaki kujua. Sitaki kusikia, sihitaji,” Zari alisema.
Aliongeza, "Jiwekee mwenyewe, sijali ni nini. Vyovyote vile nyinyi watu mnatuma katika DM yangu, tafadhali weka senti zenu mbili kwenu."
Mzazi mwenza huyo wa staa wa bongofleva Diamond Platnumz alisisitiza hamu yake ya faragha na kuwataka watu binafsi kuweka maoni yao wenyewe.
Pia aliwataka mashabiki wanaoingilia masuala yake kuzingatia maisha yao badala ya kumpa ushauri asiotakikana.
Hivi majuzi wanandoa hao walithibitisha kurudiana kwao, wiki chache tu baada ya kudokeza kuhusu matatizo ya ndoa ambayo yalidaiwa kufanya watengane.
Wanandoa hao walithibitisha kurudiana kwao Jumatano wiki jana waliposhiriki picha zao nzuri wakiwa pamoja kwenye sherehe za Umrah 2024 nchini Saudi Arabia.
Shakib alichapisha picha na video nzuri zake na mkewe kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuziambatanisha na jumbe za kupendeza na emoji za mapenzi.
"Chini ya kijani ni mahali ambapo nabii wetu mpendwa alizikwa," Shakib aliandika chini ya moja ya video alizochapisha.
Video na picha zingine ambazo kijana huyo wa miaka 32 alichapisha zilimuonyesha yeye na mkewe wakizunguka katika mji mzuri wa Riyadh nchini Saudi Arabia.
Zari pia alishiriki baadhi ya video na picha za ziara yao katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kat