Mammito anawajibu wakosoaji kuhusu video ya Jowie

Mcheshi Eunice Mammito amevunja ukimya baada ya ukosoaji kuhusu video wa kimchezo alioutengeneza dhidi ya Jowie.

Muhtasari
  • Klipu huo ulijiri saa chache baada ya Jowie kuhukumiwa kifo katika mauaji ya Monica Kimani mnamo 2018.
mammito
Mchekeshaji Eunice Mammito mammito
Image: HISANI

Mcheshi Eunice Mammito  amevunja ukimya baada ya ukosoaji kuhusu video wa kimchezo alioutengeneza dhidi ya Jowie.

Mamito alitumia mtandao wake wa kijamii Alhamisi asubuhi akisema kuwa ni nadra kwa Wakenya kuungana na kumkemea.

Klipu huo ulijiri saa chache baada ya Jowie kuhukumiwa kifo katika mauaji ya Monica Kimani mnamo 2018.

Katika video hio , anadaiwa kumshauri Jowie kuona hukumu hiyo kwa manufaa yake binafsi.

Klipu hiyo ambayo imesambaa kwa kasi imemshuhudia mcheshi huyo kupokea lawama kutoka kwa baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii.

Akijibu, Mammito amesema kwa kejeli umoja wa kumkemea unampa matumaini kuwa siku moja Wakenya wataungana kuzungumza dhidi ya maovu mbalimbali yanayoikumba nchi, ikiwemo ufisadi.

"Nimeshuhudia tukio la nadra jambo ambalo halijatokea tangu mwaka 2002 watu kutoka kila hali wakiungana kunikemea."

"Inanipa matumaini kwa siku zijazo kwamba siku moja tutaungana na kupigana dhidi ya ufisadi na mambo mengine yanayoisumbua nchi yetu", Mammito alisema.

Jibu hilo pia limevutia dhihaka, huku wengine wakimshutumu Mammito kwa kutafuta huruma baada ya fujo alizoanzisha.

Wengi walimpigia debe kwa kutojali licha ya yaliyompata Jowie, na hata kukosa kuheshimu marehemu Monica Kimani kwenye skiti yake.