Msanii Stevo Simple Boy aemfichua kwamba hali nzuri baina yake na meneja wake Chingiboy Mstado.
Kupitia instastory yake, Stevo alisema kwamba yeye na meneja wake hawako pamoja kwa sasa na kumtaka kurudi kwa ajili ya kupiga kazi pamoja kama zamani.
Msanii huyo aliweka wazi kwamba amekuwa na msongo wa mawazo kiasi kwamba anazimia akiwa anatumbuiza moja kwa moja jukwaani.
Akiwa anasikiliza wimbo wa Rose Muhando, Nimekuimbilia Bwana, Stevo alisema kwamba stress zimekuwa nyingi kwa kutorokwa na meneja na kumtaka kurudi ili waendelee kuchapa kazi.
“Meneja rudi tupige kazi, nimeishiwa nguvu. Watu wasitukosanishe. Stress inanipiga mpaka naanguka kwa stage nikiperform. Mnataka kuniharibia mpaka manager,” Stevo aliandika.
Itakumbukwa msanii huyo tangu kuondoka chini ya uongozi wa MIB, alionekana kuyumba kabla ya Chingiboy Mstado kumshika mkono na kumuongoza katika njia salama.
Akiwa chini ya Chingiboy Mstado, msanii huyo alionekana kuimarika kiasi kwamba alikutana na wabunge Peter Salasya ambaye alimhamishia maeneo salama na pia kuahidi kumjengea nyumba nzuri nyumbani kwao Oyugis.
Pia aliweza kumkutanisha na Babu Owino ambaye walifanikisha kolabo ya pamoja, Stevo, Chingiboy na Babu Owino, kwa jina Neno – wimbo ambao ulitoka wiki chache zilizopita.