Mchungaji wa kike kutoka Tanzania, Rose Shaboka amewashauri wanawake walioko katika ndoa dhidi ya kupenda kuwapigia wanaume wao kelele.
Katika moja ya klipu ya mahubiri yake, Shaboka alikuwa anawahubiria wanawake kuhusu umuhimu wa kuwapa Amani ya nafsi wanaume wao katika ndoa.
Kwa mujibu wake, korodani hazipendi kelele kabisa, kwani mwanamke anapompigia kelele mume wake, korodani zake zinasinyaa na kurudi ndani, hivyo kumfnya kuwa dhaifu.
Mchungaji huyo alitetea mahubiri yake akisema kwamba ni jambo ambalo limefanyiwa utafiti na wanasayansi.
“Na niwafundishe kina mama, kisayansi imetafitiwa na kubainika kwamba, haya mayai mawili hapa chini kwa baba hayapendi kelele, waulize madaktari watakuambia,” Shaboka alisema.
“Na unapokuwa unapiga kelele huwa yanasinyaa, kwa hiyo unapokuwa mama wa kelele unamsababishia mumewe kuwa dhaifu, hivi vitu viwili hapo chini havipendi kelele hata kidogo. Zikipigiwa kelele zinasinyaa na kuingia ndani, ulikuwa unajua hilo? Acha kelele kabisa, acha!” Shaboka alimaliza.
Hii hapa ni video ya mahubiri hayo;