Wikendi iliyopita, msanii nguli wa Afrobeats kutoka Nigeria wakati anatangaza utayarifu wa albamu yake, alitengenezwa vichwa vya habari baada ya kutoa onyo kali kwa mashabiki wake dhidi ya kuendelea kumtambua kama msanii wa Afrobeats.
Msanii huyo katika onyo hilo alisema kwamba yeye si msanii wa Afrobeats na kama kuna shabiki yeyote ambaye anamtambua kama msanii wa Afrobeats basi yuko huru kutoipakua au kuisikiliza albamu yake mpya, kwani ni Dhahiri kwamba si kwa ajili yake.
"Albamu imekamilika! Tutaonana hivi karibuni," mwimbaji wa "Loju" alianza. "Na tafadhali naomba kama unapenda Pakurumo wizkid usipakue albamu hii mpya... kwa kweli nifute kwenye orodha yako ya kucheza na maisha yako! Na kama unapenda afrobeats pls usipakue albamu yangu! Mimi si msanii wa f***ing wa afrobeats! Usiniite hivyo h*e! Mimi si Afro chochote b***h!" alisema.
Kwa jumla, kulikuwa na maoni mengi yaliyogawanyika kwa maneno haya mtandaoni, huku wengine wakikosoa tathmini yake na wengine wakitetea mtazamo wake.
Jumapili, Harmonize naye aliamka na taarifa za aina hiyo kwa mashabiki wake akikana kuwa msanii wa muziki wa Tanzania, Bongo Fleva.
Msanii huyo pia alikakiri kwamba yeye ni shabiki wa muziki huo na wala si msanii.
Msanii huyo ambaye amekuwa akitamba akijiita wa kwanza kutoka Tanzania kufanya ngoma kwa lugha ya Kiingereza na zikakubalika, aliweka ngoma yake na Bien na Bobby Shrumrda – I made it na kusema kwamba hiyo katu haiwezi kutambuliwa kama ya Bongo Fleva.
“Sawa, hapo hapo ulipo sasa hivi ingia YouTube na sehemu zozote kunakopatikana ngoma za Bongo. Ukikuta ngoma yoyote ya msanii wa Tanzania iliyoimbwa kwa Kiingereza kutoka mwaka hu, njoo chukua 10m, au kama kuna ngoma yoyote ya msanii wa Tazanania akimshirikisha msanii wa USA katika miaka 4 iliyopita, usipoikuta, basi kuanzia leo usiniite msanii wa Bongo Fleva.”
“Kwa sababu utakuwa unachanganya maji na mafuta, nyimbo zote nimekuwa nikiimba kwa lugha yangu pendwa, niite msanii wa Tanzania au Konde Boy, na hivi sina shida na mtu, kila mtu ashinde game zake, tuone mwenye mchango mkubwa,” alimaliza.