Mimi ndiye niliyeleta virusi vya corona: Nabii Owuor adai

Zaidi ya hayo, aliwaonya Wakenya dhidi ya kumpinga, akisisitiza uwezo wake wa kuleta maangamizi juu ya Kenya, ingawa alidai aliamua kuchagua neema badala yake.

Muhtasari
  • Owuor aliwaonya Wakenya dhidi ya kumpinga, akisisitiza uwezo wake wa kuleta maangamizi juu ya Kenya, ingawa alidai aliamua kuchagua neema badala yake.

Mhuburi David Owuor wa kanisa la Ministry of Repentance and holiness amedai kuwa alileta virusi vya corona ulimwenguni ili kuua wanadamu wakaidi.

Akizungumza wakati wa mahubiri katika uwanja wa Menengai mjini Nakuru Jumamosi Machi 16, Owuor alitangaza kwamba janga hilo, ambalo liligharimu maisha ya watu wengi ulimwenguni, lilitokana na maneno yake ya kinabii.

Zaidi ya hayo, aliwaonya Wakenya dhidi ya kumpinga, akisisitiza uwezo wake wa kuleta maangamizi juu ya Kenya, ingawa alidai aliamua kuchagua neema badala yake.

"Mimi ndiye niliyeleta virusi vya corona, tazama watu wangapi walikufa kwa maneno yangu. Kenya msinijaribu. Nikikuangamiza, nitakuangamiza kabisa. Lakini kwa sasa, ninakupa neema", Owuor alitangaza kwenye video.

Kauli yake ilileta hisia tofauti miongoni mwa watumiaji wa mtandao.

Hapa kuna baadhi yao:

Georgengereso: My people perish because of luck of knowledge.

daudakbari: God save the people who believe this guy is a prophet 😂

_spoilergram:Ama siri Ni kuchizi😂😂

ndumbahwinnie: Destroy us assistance jesus

quinceythedeejay: Nikama amekua content creator

parker_ndugu:Prophet or whatever you call yourself we are also tired of this Kenya destroy it

anderson_nyaberi: kwani yeye ni God

14_pixels_: Deputy holyspirit

ms.j.laura: 😂😂lol

randy_sparta:Sasa huyu anadhani tunamwogopa😂😂

kimani075: The words of the PROPHET'S OF YAHWEH come form the Lord, for those who are born again let us fear them.

hitsmoker: Hata Yesu hakuthreat watu hivo bana.