Waigizaji wa zamani wa Papa Shirandula, Jacky Vike maarufu kama Awinja na Jacquey Nyaminde maarufu Wilbroda wamefichua kwamba wanapenda sana wanaume ambao wananuka jasho ya kufanya kazi ngumu.
Katika mazungumzo na SPM Buzz wakati wa uzinduzi wa chapa moja ya bidhaa za kufua nguo, wawili hao walisema kwamba mwanamume anayenuka hivyo hiyo ndio jasho yake halali wala si jasho la uchafu.
“Mimi na Nyaminde huwa tuna shida moja, tunapenda wanaume wanaonuka ile jasho ya hadrwork. Huwa kuna kajasho Fulani, yaani ni harufu yako asili, sio jasho ya uchafu, lakini ni jasho asili hivi,” Awinja alisema huku Nyaminde akimuunga mkono.
Nyaminde kwa upande wake alichochea Zaidi akisema kwamba pia anapenda sana harufu ya wahudumu wa bodaboda.
“Mimi kwanza kuna kaharufu Fulani ka watu wa boda, kunai le inanuka vibaya lakini kuna hiyo yenye umesema ya hardwork, ile iko kama ndio alioga lakini amekuwa akifanya kazi kwa bidii siku nzima, yaani ukiwa kwa mtu wa boda halafu unamshika halafu unasikia kumuuliza ‘unaenda? Ukinidrop home si uingie hata ukunywe hata glasi ya maji’, unajua,” Nyaminde alisema huku wakicheka wote.
Wawili hao walifichua siri ya kudumu kwao kwenye tasnia ya uigizaji kwa muda mrefu ni furaha.
“Siri yetu ni furaha, huwa tunajaribu kuacha vitu vingi ambavyo vinafanyika, nikaamua sasa kusema naketi chini na kufikiria shida zangu, shida zangu ni nyingi sana kama tu za mwenzangu hapa, lakini waakti tunafikiria kwamba kuna mtu ako katika hali mbaya Zaidi, ninaambia shida zangu zikae kando, huwa hatuna shaka sana, halafu pia na maombi,” Nyaminde alisema.
Awinja naye alisema, "Mimi huwa si mtu wa titles, eti uko na cheo fulani nitakuongelesha hivi ama nitaku'treat hivi, hapana. Chukuliwa watu wote kwa usawa, kwa hiyo kuwa mkarimu kwa kila mtu."