Mwanamitindo Zari Hassan amefunguka jinsi ndoa yake imepata maboresho na mabadiliko makubwa tangu yeye na mumewe wafunge safari kwenda Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya Umrah.
Umrah ni ibada ya Waislam ambayo ni kitendo cha kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa kuingia katika hali ya Ihram, kuzunguka Nyumba, kukimbia baina ya Safa na Marwa, na kunyoa kichwa au kupunguzwa.
Mwanzoni mwa mweiz huu, Zari na mumewe Shakib walikwenda Saudi Arabia baada ya kutokea mwanya katika ndoa yao.
Baada ya kurudi kimya kimya, mshawizi huyo wa mitandaoni alitimba nchini Tanzania akiwa na mumewe bega kwa bega wakati wa uzinduzi wa chapa ya Softcare.
Japo alidinda kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yake na mumewe Saudi Arabia, mama huyo wa watoto watano alidokeza kwamba kuna mabadiliko makubwa katika ndoa yake na Shakib, tofuati na awali kabla ya kuenda Umrah.
“Unajua mimi na mume wangu tumeenda Umrah, na ilikuwa ziara nzuri sana, ilikuwa ni moja ya kubadilisha maisha na kiujumla maisha yetu sasa no tofauti kabisa,” Zari alisema.
Zari katika mahojiano na Millard Ayo awali, alikiri kwamba mambo yalikuwa mabaya sana katika ndoa yake baada ya Shakib kufungasha na kuondoka kisa video yake akiwa na baba wa wanawe, Diamond Platnumz.
Zari alisema kwa kujutia kwamba hakuweza kumtaarifu Shakib mapema kuhusu video hiyo, akisisitiza kwamba ilikuwa ni moja ya matangazo mengi ya kibiashara na wala si kurudi kwa uhusiano na Diamond, kama ambavyo pengine Shakib alifikiria kabla ya kuondoka nyumbani kkwa hasira.