Otile Brown kutumbuiza kwenye mazishi ya Brian Chira

Mwanamuziki mashuhuri, Otile Brown, ameeleza nia yake ya kufanya mazishi ya Chira kuwa tukio la kukumbukwa.

Muhtasari
  • "One Call" ya Otile ni wimbo wa moyoni unaozungumza juu ya undani wa uhusiano wa kibinadamu.
Msanii wa kizazi kipya Otile Brown katika mahojiano ndani ya Radio Jambo.
Msanii wa kizazi kipya Otile Brown katika mahojiano ndani ya Radio Jambo.
Image: Radio Jambo (Facebook)

Mwanamuziki mashuhuri, Otile Brown, ameeleza nia yake ya kufanya mazishi ya Chira kuwa tukio la kukumbukwa.

Kupitia mtandao wa instagram, Otile Brown alitangaza nia yake ya kutumbuiza wimbo wake wa One Call, unaoaminika kuwa ilikuwa wimbo Chira alipenda, bila malipo wakati wa shughuli za mazishi.

Ningependa kutumbuiza wimbo (One Call) wakati wa mazishi na kusaidia kuifanya iwe ya kukumbukwa kwake ikiwa hiyo itawezekana. Ikiwezekana, kwa watu wanaohudhuria, tafadhali mujifunze maneno ya wimbo ili tumwimbie na kumsherehekea, aliandika kwenye instastorie yake.

Instastory ya Otile Brown

"One Call" ya Otile ni wimbo wa moyoni unaozungumza juu ya undani wa uhusiano wa kibinadamu.

Hapo awali, Otile aliwaomba mashabiki waendelee kumjulisha kuhusu maandalizi ya mazishi ya Chira, akiahidi kuhudhuria mazishi.

"Nataka kusema hivi....roho yake ipumzike kwa amani.....endelea kutuhabarisha.....hatujui ni sehemu gani lakini nadhani itakuwa sahihi ikiwa tuende sisi sote kwa mazishi  ili tu kuonyesha upendo kijana huyo. Leo ni yeye ameondoka, kesho ni sisi....na wakati mwingine tunaweza kuhisi kuwa ni mbali na sisi, lakini sivyo", alisema.

Chira atazikwa Jumanne, tarehe 26 Machi 2024 huko Githunguri. Atazikwa katika vazi la kuhitimu kama alivyoomba nyanyake.